Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, akipokea zawadi kutoka kwa moja ya wagonjwa wa Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT wakati alipofanya ukaguzi wa wodi mpya za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Rais. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Idara ya huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akikagua moja ya mabasi yatakayo tumika kubeba wagonjwa wa Fistula, mabasi hayo yamenunuliwa katika mpango wa kupambana na Fistula uliochini ya CCBRT, Wizara ya Afya na Vodafone uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Februali 25.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akiwapiga picha kupitia simu yake ya mkononi watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akifurahi pamoja na watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya walemavu ya CCBRT, Dr. Wilbroad Peter Slaa akimuonyesha maendeleo ya ujenzi Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za hospitali hiyo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais Dk, Jakaya Mrisho Kikwete mapema mwezi huu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi Kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Ujenzi wa Hospitali Tom Bourel wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Dk. Jakaya Kikwete mapema Mwezi huu, Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Peter Slaa.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya wauguzi wa wodi za wagonjwa wa Fistula wa hospitali ya CCBRT, alipofanya ukaguzi wa wodi hizo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mapema Mwezi huu. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya hospitali hiyo. Dr Wilbroad Peter Slaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hii suti ya Mzee wa chadema mbona kama imemvaa.... Hata kama anaogopa kuonekana fisadi, basi atafute mitumba inayomkaa

    Ignorant

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...