Chief
Technical Advisor Youth Entrepreneurship Facility and WED -ILO Bw.
Jealous Chirove akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Kimataifa ya
Wajasiriamali uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema vijana
lazima wawe na moyo wa kujituma na kuhakikisha wanapanua wigo wa
kujiajiri wenyewe na kuondokana na fikra za kuajiriwa peke yake.
Aliongeza
kuwa ujasiriamali katika nchini kama Tanzania ni mkombozi wa pekee
katika tatizo la ajira hasa kwa vijana kwa kujiendeleza na mafunzo
mbalimbali ya ujasiriamali kama njia pekee ya kujiajiri wenyewe.
Mwenyekiti
wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for
Youth Education and Empowerment) Bw. Masoud Salim Mohamed ambao ndio
waandaaji wa maadhimisho ya wiki ya wajasiriamali inayoendea jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for
Youth Education and Empowerment) Fatma Mabrouk Khamis akielezea jinsi
alivyovutiwa kufanya maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Wajasiriamali
hapa Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kuona yanavyofanyika
nchini Marekani alikokwenda kujifunza juu ya ujasiriamali. 
Mkurugenzi
Mtendaji wa Professional Approach Group Modesta Mahiga akitoa nasaha
zake kwa vijana mbalimbali kuhusu ujasiriamali faida na changamoto zake
wakati wa maadhimisho ya wiki ya ujasiriamali hapa nchini.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Relim Entertaiment, Bi. Emelda Mwamanga Mtunga
akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya ujasiriamali ambapo
alitumia nafasi hiyo kuelezea uzoefu na changamoto za ujasirimali
nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...