Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kwa pamoja na Rais wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic, na Rais wa Baraza Kuu la Usalama kwa mwezi wa Novemba, Balozi wa India, Hardeep Singh Puri wakiwasha mishumaa, ikiwa ni ishara ya kuwaenzi na kuwakumbuka raia, wanajeshi na polisi 29 ambao wamepoteza maisha katika kipindi cha kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa Amani katika Misheni 11 za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa marehemu hao waliokumbukwa katika hafla hiyo wapo wanajeshi watatu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ambao ni Koplo Yusuf Said Chinguile, Staff Sajenti, Julius Chacha Marasi na Private Anthony Daniel Paul waliokuwa wakihudumu katika Jimbo la Darfur.
Baadhi ya wageni wakiwamo mabalozi na Waambata jeshi wakifuatilia hafla maalum ya kuwaenzi na kuwakumbuka raia, wanajeshi na polisi 29 waliopoteza maisha katika kipindi cha kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012. Hafla hiyo imefanyika siku ya Jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wengine waliopoteza maisha katika kipindi hicho wanatoka, Nigeria, Kenya, Rwanda, India, Ethiopia, Niger, Jordan, Syria, Bangladesh, Sierra leone, Senegal, Brazil, Afghanistan, Togo, Egypt.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Katibu kuu wa UN Bwana Ban Ki Moon ana shirikiana na serikali ya Rais Kikwete au ya mke wake? Kuna Jeshi la Islam na la kirsto Tanzania? Hakuna serikali Rais Kikwete hana madaraka? Kama Rais Obama? Wana danganya wananchi? Au madarka ya Rais Kikwete yako kwenye mkono wa mke wake pamoja na mafisadi? Tanzania kuna serikali au hakuna ni utawala wa mafisadi tu?

    ReplyDelete
  2. Amaaa ivi hawa watatu wanaokumbukwa hapo ndio wale tulioambiwa wamekumbwa na mafuriko walipokua wanaendesha gari na kuzolewa na maji huko darfur au? mambo mengine bwana yanatia aibu, niliishi ktk nchi fulani ulaya mashariki nilikua naona inapofika sikukuu za kuwakumbuka mashujaa wao jinsi wanavyofanya kila zuri ili kuwaletea heshima na ktk sherehe hizo huambatana na kuwaenzi maveterani ambao wangali hai, sasa kama mtu amefariki akiwa anapigania amani wewe ukasema amekumbwa na kuzolewa na mafuriko nadhani badala ya kuficha ilipaswa kuwekwa wazi ili kuleta ari na heshima si tu kwa wahanga bali hata wale walio hapa nyumbani na hasa ndio njia halisi ya kuwaonesha wananchi ghalama za kuilinda amani na si vinginevyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...