SHERIA ya kukataza ndoa za jinsia moja nchini Malawi imesitishwa kwa muda mpaka hapo uamuzi utakapotolewa na Serikali.
| Rais Banda wa Malawi: Ushoga Ruksa! |
Awali Mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi yalipigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka hadi kumi na minne jela kwa wanaokamatwa kushiriki.
Baadhi ya viongozi wa kimagharibi walitishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa kutambua haki za mashoga
Ushoga ni haramu katika nchi nyingi za Afrika na linasalia kuwa swala tete katika jamii nyingi za Afrika zenye kukumbatia maadili ya kiafrika.
Mmoja wa viongozi wa kijamii wenye ushawishi mkubwa, Kaomba, aliiomba serikali kutoruhusu bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga. ''Hii ni kinyume na maadili'' alisema kiongozi huyo.
Mnamo mwaka 2010, wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema kuwa wataoana.
Kesi hiyo ilivutia sana kero kutoka kwa jamii ya kimataifa na hata kusababisha baadhi ya wahisani kusitisha msaada kwa nchi hiyo, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.
Rais wakati huo akiwa , Bingu wa Mutharika - aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na tamaduni za kiafrika na hata sheria za nchi.
Hata hivyo Rais Joyce Banda, aliyemrithi Bingu aliwaambia wabunge kuwa anataka kubatilisha sheria hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.


Huyu mama ni kibaraka wa Uingereza na Marekani.
ReplyDeleteduh sijui ni wapi tunapoelekea dunia sasa inatisha sana hizi ni dalili zote za mwisho wa dunia.
ReplyDeleteNjaa mbaya...masharti hayo ya wanao waweka mujini
ReplyDeletewaafrika tutaacha lini kufuata tabia za wazungu? tunasahau mila na desturi zetu na tunaona kila afanyalo mzungu ndio sawia!!!!!
ReplyDeleteHiyo ni njaa tu. Wanaogopa kunyimwa misaada.
ReplyDeletewawaekeni wanawake juu ni madhara yake hayoooo mnaanza kuyaona.
ReplyDeleteWewe mdau hapo juu! Wanaume wangapi wameachia rasilimali muhimu za Taifa kwa ulaku, uchoyo na tamaa sembuse wanaotaka ushoga! Shida yako nini bwana! Huo ni uamuzi wa mtu binafsi!
ReplyDeleteKwa si upo tu na unafanyika kwa siri!
Nchi itanuka kinyesi! Na wewe mdau unaesema kuwa huo ni uamuzi wa mtu binafsi bora ungekwenda mapema kuomba uraia Malawi kwa sababu hapa tutakuwa tunakubugudhi.
ReplyDeleteSafii sana Anonymous wa Fri Nov 09, 08:33:00 PM 2012 siye wabongo tumezoea unafiki. Utakandamizaje wanawake wote kwa shida wanazopata kwa fujo zetu sisi wanaume? Africa itakapoanza kumnyanyua mwanamke wake ndipo tutaendelea bila hivyo ni magumashi tu.
ReplyDeleteall in the name of msaada tunamkufuru Mwenyezi Mungu, we'll see nani bora msaada au Mwenyezi Mungu.
ReplyDeleteWamalawi kujikomba kwa wazungu ni kitu kiko kwenye damu zao. Hata raisi wao wa kwanza alipingana na akina Nyerere waliokuwa waongoza harakati za ukombozi wa weusi wenzetu kusini ili wasiendelee kukandamizwa na vitimoto, yeye aliwasapoti.
ReplyDeleteNgoja nikaoe mwanaume wa kimalawi, kumbe kwao ruksa.
ReplyDeleteItabidi tuwaoe hawa halafu ndio tuwape ziwa Nyasa lote na kuwaruhusu kuliita Lake Malawi, mchezo utakuwa umeisha.
ReplyDeleteAlaaaaa kumbe anayewapa kichwa Malawi kudai Ziwa Nyasa ni Uingereza!
ReplyDeleteSi mnaona yale yale Mashariti ya Misaada ya Uingereza tuliyoyakataa wao Malawi wameyakubali nadhani wameahidiwa na hiyo hiyo Uingereza kusaidiwa hata kulidai Ziwa Nyasa liwe lao!
Wale Mashoga wa kariakoo na pale zanzibar wameruhusiwa na nani?
ReplyDeleteHuyu mama njaa kali sana,
ReplyDeleteNdio maana ameshindwa kuwahudumia watu wake kwa njaa na sasa amewauza kwa Uingereza kuruhusu walawitiwe ili wasaidiwe !
Na huku anatapa tapa analitaka Ziwa!
Malawi kama wanataka Ziwa Nyasa na sisi tuwape MASHARITI YA WAMALAWI WANAUME WAOLEWE TANZANIA!
ReplyDeleteSI WAMEIKUBALIA UINGEREZA KWA NINI ISIWE SISI AMBAKO WAO WANAKOHITAJI KITU?
Ahaaa madai yao ya kutaka Ziwa Nyasa liwe lao kumbe hawa wana akili za 'Upunga' sio?
ReplyDeleteSasa tukivua samaki kwenye ziwa nyasa na tukiona samaki Huyo kalegea basi tumrudishe kwao Malawi. na samaki alikomaa wetu Huyo.
ReplyDelete