SHERIA ya kukataza ndoa za jinsia moja nchini Malawi imesitishwa kwa muda mpaka hapo uamuzi utakapotolewa na Serikali.


Rais Banda wa Malawi: Ushoga Ruksa!
Serikali ililiagiza jeshi la polisi kutowakamata watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja , mpaka hapo uamuzi utakapotolewa rasmi na Serikali.


Awali Mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi yalipigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka hadi kumi na minne jela kwa wanaokamatwa kushiriki.


Baadhi ya viongozi wa kimagharibi walitishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa kutambua haki za mashoga


Ushoga ni haramu katika nchi nyingi za Afrika na linasalia kuwa swala tete katika jamii nyingi za Afrika zenye kukumbatia maadili ya kiafrika.


Mmoja wa viongozi wa kijamii wenye ushawishi mkubwa, Kaomba, aliiomba serikali kutoruhusu bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga. ''Hii ni kinyume na maadili'' alisema kiongozi huyo.


Mnamo mwaka 2010, wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema kuwa wataoana.


Kesi hiyo ilivutia sana kero kutoka kwa jamii ya kimataifa na hata kusababisha baadhi ya wahisani kusitisha msaada kwa nchi hiyo, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.


Rais wakati huo akiwa , Bingu wa Mutharika - aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na tamaduni za kiafrika na hata sheria za nchi.


Hata hivyo Rais Joyce Banda, aliyemrithi Bingu aliwaambia wabunge kuwa anataka kubatilisha sheria hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Huyu mama ni kibaraka wa Uingereza na Marekani.

    ReplyDelete
  2. duh sijui ni wapi tunapoelekea dunia sasa inatisha sana hizi ni dalili zote za mwisho wa dunia.

    ReplyDelete
  3. Njaa mbaya...masharti hayo ya wanao waweka mujini

    ReplyDelete
  4. waafrika tutaacha lini kufuata tabia za wazungu? tunasahau mila na desturi zetu na tunaona kila afanyalo mzungu ndio sawia!!!!!

    ReplyDelete
  5. Hiyo ni njaa tu. Wanaogopa kunyimwa misaada.

    ReplyDelete
  6. wawaekeni wanawake juu ni madhara yake hayoooo mnaanza kuyaona.

    ReplyDelete
  7. Wewe mdau hapo juu! Wanaume wangapi wameachia rasilimali muhimu za Taifa kwa ulaku, uchoyo na tamaa sembuse wanaotaka ushoga! Shida yako nini bwana! Huo ni uamuzi wa mtu binafsi!
    Kwa si upo tu na unafanyika kwa siri!

    ReplyDelete
  8. Nchi itanuka kinyesi! Na wewe mdau unaesema kuwa huo ni uamuzi wa mtu binafsi bora ungekwenda mapema kuomba uraia Malawi kwa sababu hapa tutakuwa tunakubugudhi.

    ReplyDelete
  9. Safii sana Anonymous wa Fri Nov 09, 08:33:00 PM 2012 siye wabongo tumezoea unafiki. Utakandamizaje wanawake wote kwa shida wanazopata kwa fujo zetu sisi wanaume? Africa itakapoanza kumnyanyua mwanamke wake ndipo tutaendelea bila hivyo ni magumashi tu.

    ReplyDelete
  10. all in the name of msaada tunamkufuru Mwenyezi Mungu, we'll see nani bora msaada au Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete
  11. Wamalawi kujikomba kwa wazungu ni kitu kiko kwenye damu zao. Hata raisi wao wa kwanza alipingana na akina Nyerere waliokuwa waongoza harakati za ukombozi wa weusi wenzetu kusini ili wasiendelee kukandamizwa na vitimoto, yeye aliwasapoti.

    ReplyDelete
  12. Ngoja nikaoe mwanaume wa kimalawi, kumbe kwao ruksa.

    ReplyDelete
  13. Itabidi tuwaoe hawa halafu ndio tuwape ziwa Nyasa lote na kuwaruhusu kuliita Lake Malawi, mchezo utakuwa umeisha.

    ReplyDelete
  14. Alaaaaa kumbe anayewapa kichwa Malawi kudai Ziwa Nyasa ni Uingereza!

    Si mnaona yale yale Mashariti ya Misaada ya Uingereza tuliyoyakataa wao Malawi wameyakubali nadhani wameahidiwa na hiyo hiyo Uingereza kusaidiwa hata kulidai Ziwa Nyasa liwe lao!

    ReplyDelete
  15. Wale Mashoga wa kariakoo na pale zanzibar wameruhusiwa na nani?

    ReplyDelete
  16. Huyu mama njaa kali sana,

    Ndio maana ameshindwa kuwahudumia watu wake kwa njaa na sasa amewauza kwa Uingereza kuruhusu walawitiwe ili wasaidiwe !

    Na huku anatapa tapa analitaka Ziwa!

    ReplyDelete
  17. Malawi kama wanataka Ziwa Nyasa na sisi tuwape MASHARITI YA WAMALAWI WANAUME WAOLEWE TANZANIA!

    SI WAMEIKUBALIA UINGEREZA KWA NINI ISIWE SISI AMBAKO WAO WANAKOHITAJI KITU?

    ReplyDelete
  18. Ahaaa madai yao ya kutaka Ziwa Nyasa liwe lao kumbe hawa wana akili za 'Upunga' sio?

    ReplyDelete
  19. Sasa tukivua samaki kwenye ziwa nyasa na tukiona samaki Huyo kalegea basi tumrudishe kwao Malawi. na samaki alikomaa wetu Huyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...