Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kuhusu taarifa ya mapato na matumizi katika kipindi cha miezi mitatu ya kuwapo kwao madarakni (Julai 15 hadi Oktoba 15, mwaka huu),  Wengine kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Yanga, Dennis Oundo na kushoto Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako. Katika taarifa hiyo, inaonyesha Yanga ilitumia Sh. Milioni 375 kwa usajili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bravo yanga! Sijawahi kuona timu hii na mkubwa mwenzake Simba wakitoa taarifa za mahesabu yao!!! Ishara nzuri kwamba kweli kuna mabadiliko ya uongozi!!!

    Ingekuwa vizuri zaidi kuwa na maelezo sahihi za zile milioni zilizotumika pasipo maelezo. (magazeti ya jana yameeleza)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...