Dah! Hata sijui niseme nini. Kuhama sihami (kwangu Bwawa ni kama kabila, sio dini ama utaifa) lakini hamu sina kwa jinsi gundu linavyotuelemea Bwawa la Maini, kiasi hata kuangalia mechi siku hizi ni kwa nadra sana, achilia mbali kuzungumzia, kwani tukishinda gemu moja leo ujue mechi tatu zijazo kama sio droo basi kichapo. Nani katuroga wajameni??? Yaani katika gemu 19 tumeshinda 6 na droo 7, hii kweli ni haki jamani??? Halafu kwenye nafasi tuko wa 10 hadi dakika hii. Sijui nijitungike...Ah, nshachoka mie!
Iko haja ya kuunga mkono mdau mmoja aliyeshauri nihamie kwingine kwa mkopo hadi mambo yatapokuwa mazuri Bwawani (Sijui lini hiyo) ila tatizo sijui nihamie chama gani kwa sasa kwa mkopo. Ushauri tafazali...
Iko haja ya kuunga mkono mdau mmoja aliyeshauri nihamie kwingine kwa mkopo hadi mambo yatapokuwa mazuri Bwawani (Sijui lini hiyo) ila tatizo sijui nihamie chama gani kwa sasa kwa mkopo. Ushauri tafazali...
Kama hadi Ankol amekubali kuwa mambo ni magumu basi kweli ni magumu. Chukua moyo mgumu wa Wenger utaona maisha ni poa, maana yeye kufungwa ashazoea sasa.
ReplyDeleteSaga chupa umeze! pambaf! na mbado!
ReplyDeleteAnkal wewe km mimi haiwezekaniki kuhama ndo tumo tu na jahazi letu.lakini iko siku tutafurahi km zamani
ReplyDeleteNjoo Manchester Unt kwa mkopo mpaka mambo yakishakuwa swafi bwawa la maini then utarudi.
ReplyDeletemmeruka dhahabu mmekanyaga mavi,wale masheikh wa dubai walitaka kuinunua il mkaona bora wale wamarekani watapeli, matokeo yake ndio hayo mnaambulia kununua wachezaji wa sumni sumni na kichapo kama kawa.
ReplyDeletehahami mtu tutashuka nayo na kupanda nayo
ReplyDeleteMwe! bora mshauriane kutohama wajameni, unaweza kukuta gundu liko kwenu washabiki mkahamia huku kwetu na sie mambo yakaanza kwendamrama....
ReplyDeleteShetani mwekundu.
Ankal pole sana ,njoo kwa mkopo stanford darajani mambo yakiwa safi utarudi kwako ila kama huna ugonjwa wa moyo basi vumilia kaka
ReplyDeleteNjoo Yanga, tena BUREEEEE!
ReplyDeleteImetabiriwa kuwa Liverpool, ambayo ilitwaa taji lake la mwisho ya Ligi Kuu ya England mwaka 1990, itashinda tena taji hilo mwakja 2050.
ReplyDelete