Dah! Hata sijui niseme nini. Kuhama sihami (kwangu Bwawa ni kama kabila, sio dini ama utaifa)  lakini hamu sina kwa jinsi gundu linavyotuelemea Bwawa la Maini, kiasi hata kuangalia mechi siku hizi ni kwa nadra sana, achilia mbali kuzungumzia, kwani tukishinda gemu moja leo ujue mechi tatu zijazo kama sio droo basi kichapo. Nani katuroga wajameni??? Yaani katika gemu 19 tumeshinda 6 na droo 7, hii kweli ni haki jamani??? Halafu kwenye nafasi tuko wa 10 hadi dakika hii. Sijui nijitungike...Ah, nshachoka mie!
Iko haja ya kuunga mkono mdau mmoja aliyeshauri nihamie kwingine kwa mkopo hadi mambo yatapokuwa mazuri Bwawani (Sijui lini hiyo) ila tatizo sijui nihamie chama gani kwa sasa kwa mkopo. Ushauri tafazali...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kama hadi Ankol amekubali kuwa mambo ni magumu basi kweli ni magumu. Chukua moyo mgumu wa Wenger utaona maisha ni poa, maana yeye kufungwa ashazoea sasa.

    ReplyDelete
  2. Saga chupa umeze! pambaf! na mbado!

    ReplyDelete
  3. Ankal wewe km mimi haiwezekaniki kuhama ndo tumo tu na jahazi letu.lakini iko siku tutafurahi km zamani

    ReplyDelete
  4. Njoo Manchester Unt kwa mkopo mpaka mambo yakishakuwa swafi bwawa la maini then utarudi.

    ReplyDelete
  5. mmeruka dhahabu mmekanyaga mavi,wale masheikh wa dubai walitaka kuinunua il mkaona bora wale wamarekani watapeli, matokeo yake ndio hayo mnaambulia kununua wachezaji wa sumni sumni na kichapo kama kawa.

    ReplyDelete
  6. hahami mtu tutashuka nayo na kupanda nayo

    ReplyDelete
  7. Mwe! bora mshauriane kutohama wajameni, unaweza kukuta gundu liko kwenu washabiki mkahamia huku kwetu na sie mambo yakaanza kwendamrama....
    Shetani mwekundu.

    ReplyDelete
  8. Ankal pole sana ,njoo kwa mkopo stanford darajani mambo yakiwa safi utarudi kwako ila kama huna ugonjwa wa moyo basi vumilia kaka

    ReplyDelete
  9. Njoo Yanga, tena BUREEEEE!

    ReplyDelete
  10. Imetabiriwa kuwa Liverpool, ambayo ilitwaa taji lake la mwisho ya Ligi Kuu ya England mwaka 1990, itashinda tena taji hilo mwakja 2050.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...