Tarehe 18 Januari 2012, Hospitali ya Taifa Muhimbili ilimpokea “Esther Meshaki” baada ya kutoka kwa Polisi waliodai kumuokota barabarani katika eneo la Temeke. Inadaiwa kuwa mgonjwa huyu alikuwa hawezi kuongea. Watalaam wetu wamejitahidi kutoa huduma kwa mgonjwa huyu kufikia kiwango cha kuweza kuongea mwenyewe na kujitambua vizuri.
Changamoto tuliyonayo ni kuwa mgonjwa huyu tangu alazwe hakuna ndugu wala jamaa yake yeyote aliyejitokeza. Hivyo kwa sasa tunatafuta ndugu wa mgonjwa huyu ambaye amepata nafuu ili aweze kujiunga na familia yake.
Katika kufanya udadisi inaonekana kuwa Esther Meshaki alizaliwa Kigoma Vijijini katika Kijiji cha Kigogwe miaka ya 1985. Kabila lake ni Muha.
Esther anasema mama yake anaitwa Dotto Alfred na Baba yake anaitwa Meshaki Alfred.
Hata hivyo Esther anadai wazazi wake walitengana na baada ya kutengana
yeye na mama yake mzazi waliahamia Morogoro katika Kijiji cha Nguru wa Ndege (Nguruka). Inaonekana Esther akifika eneo linaloitwa Sabasaba lililopo nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro anaweza kufika nyumbani kwao kama yeye anavyodai Esther alitueleza kuwa ana mtoto mwenye umri wa miaka miwili aitwaye Clemensia Mlenda ambaye alimzaa na kijana aitwaye Mlenda katika Kijiji cha Nguru.
Alikujaje Dar es Salaam
Katika kufanya udadisi, na kuongea naye inaonekana alikuja kufanya kazi za ndani lakini hajuhi ni wapi alipokuwa akifanya kazi hiyo hapa Jijini.
Kwa hiyo tunaomba yeyote anayemfahamu Esther, au ndugu wa Esther
ajitokeze ili kutupatia taarifa sahihi tuweze kumrudisha nyumbani kwao na akajiunge na familia yake.
Tafadhali yeyote mwenye taarifa zake naomba awasiliane na Ofisi ya Uhusiano kupitia namba 0755 64 86 36.
Mkuu uhusiano muhimbili ungeweka picha yake. labda majirani au wauza duka wangeweza kutoa taarifa ya familia alikokua anafanya kazi.
ReplyDelete