Mwanamuziki mahiri ndani ya kundi la Quartie Latin aitwae Cindy, linaloongozwa na nyota wa muziki wa dansi kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akiimba jukwaani usiku huu  mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa wingi (hawapo pichani),kwenye tamasha la usiku wa Tusker Carnival ndani ya viwanja vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
 Mwanamuziki Koffi Olomide akijimwaya mwaya kwa madaha kabisa jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Tusker Carnival,huku akishangiliwa na umati mkubwa watu uliohudhuria tamasha hilo.

 Pichani juu na chini ni Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide sambamba na skwadi lake la Quartie Latin
 Koffi Olomide akimtambulisha rafiki yake mkubwa jukwaani,Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga,ambaye ndiye aliyemleta hapa nchini kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya  bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker,ambapo pia mwanamuziki huyo alimshukuru sana Joseph kusaga kwa ukarimu wake
 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,akizungumza machache na kuwashukuru sana wadhamini wa onesho hilo sambamba na wadau mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye onesho hilo ambalo limefana kwa kiasi kikubwa.Picha zaidi BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi! Nashukuru kwa kionjo ilichokiweka basi nasi tuliopo nje angalau tuwekee hizo ngoma hata kwa dakika 15 tuweze kufurahia kama nyie mulivyofaidi hapo bongo,hii ni pia na onyesho la JB MPIANA alipokuwa hapo bongo novemba.

    ReplyDelete
  2. Hatari lakini salama hapo jukwaani

    ReplyDelete
  3. Ce n'est pas Quartie Latin c'est Quartier Latin. Usiharibu jina la band. SC - Mdau Toronto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...