Waziri wa Uchukuzi leo mchana amezindua rasmi usafiri wa treni za
abiria toka Dar es Salaam hadi Mwanza, hivyo kutimiza ahadi ya
Serikali iliyotolewa Bungeni kipindi cha Bajeti mwaka huu kuhusu
kurejesha huduma hiyo.
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa amefuatana na
viongozi wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara, Injinia Omar Chambo
na Mtendaji Mkuu wa TRL, Injinia Kipallo kisamfu aliruhusu treni hiyo
kuondoka stesheni ya Dar es Salaam Saa 8:30 mchana huku abiria
wakishangilia na kudai huduma hiyo iendelezwe zaidi na zaidi.
Usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar na Mwanza ulisitishwa Desemba
2009 kufuatia maamuzi ya iliyokuwa menejimenti ya Kampuni ya RITES
kutoka India .
Treni hiyo ikiwa imefunga Mabehewa 16 yenye abiria wapatao elfu moja
inatarajiwa kuingia Mwanza Jumapili asubuhi na kupokewa na Mhe. Naibu
Waziri wa UCHUKUZI, Dkt. Charles Tizeba na viongozi mbalimbali wa mkoa
wa Mwanza.
Akiongea na viongozi na Wafanyakazi baada ya ufunguzi huo, Dkt.
Mwakyembe aliwapongeza Wafanyakazi wa TRL hasa mafundi wa karakana za
Dsm na Morogoro kwa kazi kubwa ya kufufua Injini na Mabehewa hivyo
kulikolea Taifa mabilioni ya pesa ambazo zingetumika kukodisha vifaa
hivyo kutoka Afrika ya Kusini, India ama nchi nyingine.
Treni ya abiria ya Mwanza itakuwepo kwa kuanzia mara mbili kwa wiki
Jumanne na Ijumaa kama ilivyo kwa treni ya Kigoma na baadaye
kuongezeka jinsi injini na mabehewa yatakavyokuwa yanaongezeka
kutengenezwa.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa kuanza tena kwa safari za treni ya abiria kwenda Mwanza.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akizungumza na Uongozi wa TRL na baadhi ya Wanareli mara baada ya uzinduzi wa treni kwenda Mwanza katika stesheni ya Dar.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe mwenye suti akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kabla kuzindua safari ya treni ya abiria kwenda Mwanza leo mchana katika Stesheni ya Dar es Salaam.
Hongera Dk.Mwakyembe!
ReplyDeleteMH.Mwakyembe,tunakushukuru sana kwa juhudi zako za kuimarisha usafiri wa reli ya kati.Tafadhali sana angalia uwezekano wa kupata engine zingine za treni,zilizopo zimechoka,abiria wanapata usumbufu wa kulala maporini kwa ajili ya ubovu wa engine.Mungu akupe nguvu endelea na kuchapa kazi.
ReplyDeleteMwakyembe Jamani sijui nikupe nini Mzalendo wewe kwa kweli kwa haya unayofanya umenigusa kweli!
ReplyDeleteJamani Watanzania wote mnaojua maana ya haya anayofanya Mwakyembe hebu njooni na mawazo yenu.
Mimi binafsi kwa kweli nimefarijika sana kwa hili maaana ni njia kama hizi tu ndiyo zinaweza kuturekebishia uchumi wetu na kupunguza gharama za maisha kwa Watanzania wa kipato cha chini.
BRAVO BOROTHER MWAKYEMBE GOD BLESS YOU!!!!!!!!!!.
Go go go Mwakyembe......
ReplyDelete