Waziri wa Uchukuzi leo mchana amezindua rasmi usafiri wa treni za abiria toka Dar es Salaam hadi Mwanza, hivyo kutimiza ahadi ya Serikali iliyotolewa Bungeni kipindi cha Bajeti mwaka huu kuhusu kurejesha huduma hiyo. 
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa amefuatana na viongozi wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara, Injinia Omar Chambo na Mtendaji Mkuu wa TRL, Injinia Kipallo kisamfu aliruhusu treni hiyo kuondoka stesheni ya Dar es Salaam Saa 8:30 mchana huku abiria wakishangilia na kudai huduma hiyo iendelezwe zaidi na zaidi. 
 Usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar na Mwanza ulisitishwa Desemba 2009 kufuatia maamuzi ya iliyokuwa menejimenti ya Kampuni ya RITES kutoka India . 
 Treni hiyo ikiwa imefunga Mabehewa 16 yenye abiria wapatao elfu moja inatarajiwa kuingia Mwanza Jumapili asubuhi na kupokewa na Mhe. Naibu Waziri wa UCHUKUZI, Dkt. Charles Tizeba na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza. 
 Akiongea na viongozi na Wafanyakazi baada ya ufunguzi huo, Dkt. Mwakyembe aliwapongeza Wafanyakazi wa TRL hasa mafundi wa karakana za Dsm na Morogoro kwa kazi kubwa ya kufufua Injini na Mabehewa hivyo kulikolea Taifa mabilioni ya pesa ambazo zingetumika kukodisha vifaa hivyo kutoka Afrika ya Kusini, India ama nchi nyingine. 
 Treni ya abiria ya Mwanza itakuwepo kwa kuanzia mara mbili kwa wiki Jumanne na Ijumaa kama ilivyo kwa treni ya Kigoma na baadaye kuongezeka jinsi injini na mabehewa yatakavyokuwa yanaongezeka kutengenezwa.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa kuanza tena kwa safari za treni ya abiria kwenda Mwanza.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akizungumza na Uongozi wa TRL na baadhi ya Wanareli mara baada ya uzinduzi wa treni kwenda Mwanza katika stesheni ya Dar.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe mwenye suti akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kabla kuzindua safari ya treni ya abiria kwenda Mwanza leo mchana katika Stesheni ya Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera Dk.Mwakyembe!

    ReplyDelete
  2. MH.Mwakyembe,tunakushukuru sana kwa juhudi zako za kuimarisha usafiri wa reli ya kati.Tafadhali sana angalia uwezekano wa kupata engine zingine za treni,zilizopo zimechoka,abiria wanapata usumbufu wa kulala maporini kwa ajili ya ubovu wa engine.Mungu akupe nguvu endelea na kuchapa kazi.

    ReplyDelete
  3. Mwakyembe Jamani sijui nikupe nini Mzalendo wewe kwa kweli kwa haya unayofanya umenigusa kweli!

    Jamani Watanzania wote mnaojua maana ya haya anayofanya Mwakyembe hebu njooni na mawazo yenu.

    Mimi binafsi kwa kweli nimefarijika sana kwa hili maaana ni njia kama hizi tu ndiyo zinaweza kuturekebishia uchumi wetu na kupunguza gharama za maisha kwa Watanzania wa kipato cha chini.

    BRAVO BOROTHER MWAKYEMBE GOD BLESS YOU!!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  4. Go go go Mwakyembe......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...