Na Mwandishi wetu
Giza lililotanda kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Emmenuel Okwi limefikia kikomo baada ya klabu hiyo kusaini mkataba wa miaka miwili.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaji Ismail Aden Rage alisema mara baada ya kuwasili jijini jana kuwa kutokana na usajili huo, sasa Okwi ataichezea timu hiyo zaidi ya miaka miwili kutokana na ukweli kuwa mkataba wake wa awali ulikuwa haujamalizika.
Rage alisema kuwa kusaini kwa Okwi ni kumaliza vita waliyokuwa nao dhidi ya vilabu vingine vilivyokuwa vikihaha kumsajili mchezaji huyo katika kila kona kwa dau nono.
“Haikuwa kazi rahisi kumsajili mchezaji  huyu, tumeyumbishwa sana na klabu nyingine, tunamshukuru kwa kukubali sera zetu na sasa kujifunga kwa miaka miwili,” alisema Rage na kutamba kuwa wataanza mzunguko wa pili kwa kishindo na kutetea vyema ubingwa wao.
Kuhusiana na Sunzu, Rage alisema kuwa mchezaji huyo hawezi kuichezea timu hiyo kutokana na majeraha aliyokuwa nayo  yeye mwenyewe kuamua kukatisha mkataba. Alisema kuwa wataangalia hali itakavyokuwa kama wamlipishe fedha kwa kufikia uamuzi huo au la.
“Sunzu ni mgonjwa na wala hafanyi ujanja wa kutaka tumwachie ajiunge na timu nyingine, anatia huruma sana, nini tutafanya kutokana na hili, tutatangaza hapo baadaye,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Okwi mwoneni hapo kwenye picha kichwa chake kina kona kama sambusa utosini akiwa na Kijunju cha kichwani kama Jongoo au ndege wao Crane wa Uganda !!!

    Hata mkisema mimi namnanga Okwi vile mimi ni Yanga ndio , mimi ni Yanga natumia nafasi yangu kama Mtani wa Simba S.C., au hamtaki?

    ReplyDelete
  2. Hahahahahaha!

    Okwi Raia wa Uganda ana 'kijunju' kichwani kama ndege wa kwao CRANE!

    ahhh Wabongo masihara mnayaweza!

    Mwenyewe Okwi akisikia patakuwa salama?

    ReplyDelete
  3. Ohhh


    Mdau wa kwanza umesema kweli!

    Jamaa Okwi ana kichwa cha jogoo kabisa hata ukiangalia hiyo picha hapo kinaonekana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...