Na Mwandishi wetu
Giza lililotanda kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Emmenuel Okwi limefikia kikomo baada ya klabu hiyo kusaini mkataba wa miaka miwili.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaji Ismail Aden Rage alisema mara baada ya kuwasili jijini jana kuwa kutokana na usajili huo, sasa Okwi ataichezea timu hiyo zaidi ya miaka miwili kutokana na ukweli kuwa mkataba wake wa awali ulikuwa haujamalizika.
Rage alisema kuwa kusaini kwa Okwi ni kumaliza vita waliyokuwa nao dhidi ya vilabu vingine vilivyokuwa vikihaha kumsajili mchezaji huyo katika kila kona kwa dau nono.
“Haikuwa kazi rahisi kumsajili mchezaji huyu, tumeyumbishwa sana na klabu nyingine, tunamshukuru kwa kukubali sera zetu na sasa kujifunga kwa miaka miwili,” alisema Rage na kutamba kuwa wataanza mzunguko wa pili kwa kishindo na kutetea vyema ubingwa wao.
Kuhusiana na Sunzu, Rage alisema kuwa mchezaji huyo hawezi kuichezea timu hiyo kutokana na majeraha aliyokuwa nayo yeye mwenyewe kuamua kukatisha mkataba. Alisema kuwa wataangalia hali itakavyokuwa kama wamlipishe fedha kwa kufikia uamuzi huo au la.
“Sunzu ni mgonjwa na wala hafanyi ujanja wa kutaka tumwachie ajiunge na timu nyingine, anatia huruma sana, nini tutafanya kutokana na hili, tutatangaza hapo baadaye,” alisema.
Okwi mwoneni hapo kwenye picha kichwa chake kina kona kama sambusa utosini akiwa na Kijunju cha kichwani kama Jongoo au ndege wao Crane wa Uganda !!!
ReplyDeleteHata mkisema mimi namnanga Okwi vile mimi ni Yanga ndio , mimi ni Yanga natumia nafasi yangu kama Mtani wa Simba S.C., au hamtaki?
Hahahahahaha!
ReplyDeleteOkwi Raia wa Uganda ana 'kijunju' kichwani kama ndege wa kwao CRANE!
ahhh Wabongo masihara mnayaweza!
Mwenyewe Okwi akisikia patakuwa salama?
Ohhh
ReplyDeleteMdau wa kwanza umesema kweli!
Jamaa Okwi ana kichwa cha jogoo kabisa hata ukiangalia hiyo picha hapo kinaonekana!