maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu yaliyohusisha Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali, Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu yakiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Mgeni rasmi Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisoma hotuba yake ambapo amesema Pamoja na kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Haki za Binadamu, pia tunaadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa pamoja. Kaulimbiu ya mwaka huu katika Kupambana na Rushwa ni “Unaweza kuzuia rushwa, chukua hatua sasa”. Kauli hii inaonesha umuhimu wa Wananchi wa rika zote kupiga vita rushwa.

Mh. Pinda amesema hatua ya kuunganisha maadhimisho haya na kufanyika sehemu moja kunapunguza gharama kwa upande wa Serikali, na pia kunatoa nafasi kwa Wananchi kufahamu umuhimu wa siku zote mbili bila kulazimika kuondoka eneo moja la tukio kwenda eneo jingine. Napenda kuzipongeza Taasisi zote husika kwa kuunganisha matukio haya mawili na kuadhimisha sehemu moja na kwa wakati mmoja.

Ameongeza kuwa Huu ni mwaka wa tano tangu Taifa letu lilipoanza kuadhimisha siku hii Kitaifa. Kaulimbiu ya Kimataifa kwa mwaka huu ni: “Sauti yangu inachangia” (My voice counts). Ujumbe huu unatukumbusha kushiriki katika kutoa maoni katika shughuli mbalimbali za Kijamii au Kitaifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Waziri Mkuu Pinda kuendelea kuelimisha wananchi kuhusu haki za binadamu kwa vitendo.Uwaji wa ALBINO unta endelea kumfata Rais Kikwete.Hata weza kuwa dhulumu haki za ALBINO kwa kufuguwa shule, barabara au hospitali ya watoto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...