Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na meneja wa Wings of Kilimanjaro Bi Paula McRae jijini Arusha hivi karibuni. 

Wings of Kilimanjaro, tukio linalotokea mara moja katika maisha, linategemea kufanyika mwishoni mwa Januari 2013, ambapo kiasi cha watu 200, ambao  watalaamu wa spoti inayoitwa ‘paragliding’ (vishada vinavyobeba watu) and ‘philanthropists’ (wachangiaji wa misaada kwa jamii)  wanatarajiwa kufika  na kupaa juu  kilele cha Mlima Kilimanjaro, ambapo nia ya tukio hili ni kukusanya  dola millioni moja za Kimarekani kusaidia taasisi tatu ambazo zinafanya kazi ya kusaidia jamii hapa Tanzania, ambazo  ni ‘Plant With Purpose’, ‘One Foundation’ na ‘World Serve International’.
  Katika siku ya uzinduzi, wataalamu wa paragliding (ikiwemo wale amabyo wanajulikana duniani) na abiria wao watazindua siku hiyo na kwenda eneo la Moshi ambapo watatua. Muda wa kuruka angani mpaka Moshi ni takriban  dakika 40.  
Hivi karibuni, Meneja wa Wings of Kilimanjaro, Bi Paula McRae, alipata nafasi ya kukutana na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika safari yake huko Arusha. Alipokuwa anaongea naye kuhusu tukio la Wings of Kilimanjaro, Rais Kikwete  alifurahi sana na aliwashukuru kwa timu ya Wings of Kilimanjaro kwa kutoa ushirikiano na kwa juhudi zao za  kutafuta fedha na pia kuweza kupromote Mt. Kilimanjaro ulimwenguni. 
Rais aliendelea kutambua habari katika vyombo vya habari ikizungumzia boti ya Mt. Kilimanjaro ambayo ilikuwepo London, nchini Uingereza (zaidi ya watu milioni 20 wanaangalia katika kipindi cha BBC), pia iliweza kutoka kwenye magazine ya National Geographic na pia kupokelewa na balozi wa hiari wa Utalii Tanzania,Bw. Doug Pitt. 

Bi Paula McRae amesema timu ya Wings of Kilimanjaro wanafurahia kuwaonyesha kwa Watanzania mchezo huo wa Paragliding ambao haijulikani sana nchini, na kwamba timu ya Wings of Kilimanjaro itatoa ushindani wakikaribia katika tukio na kwamba Watanzania wawili watapata fursa ya  kusafiri na rubani wa paragliding mwezi wa pili.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hili ni tukio la kipekee kwa Tanzania Kama ilivyo kwa maajabu Saba ya Dunia ambapo Tanzania imepata nafasi ya Mlima Kilimanjaro kuwania nafasi ya kushinda. Tanzania tusisubiri watu wa nje wavipe handi vya kwetu bila sisi kuanza na wnapoanza basi kwa nguvu zote tujitahidi Kuiteka nafasi hiyo ili kweli cha kwetu kipate thamani. Pia makampuni ya kizalendo yajitokeze kudhamini mambo kama haya ili kweli Tanzania isikike mfano mzuri ni Afrika Kusini na Kombe la dunia, japo wageni walikimbilia kudhamini lakini wazalando walijiunga na kuhakikisha wao ndo wanaitangaza nchi yao zaidi. Tuthamini vyakwetu Tanzania

    ReplyDelete
  2. mh mdada sio mchezo moto wa kuotea mbali

    ReplyDelete
  3. mmh dadangu wee chonde naka blauzi hako!

    ReplyDelete
  4. Huyu mdada naye vipi? Kumkalia Rais wetu mpendwa kifua wazi, anataka nini?

    ReplyDelete
  5. Makubwa!, hapa ilikuwa kazi kweli kweli kujaribu ku-focus ktk tukio hili muhimu kwa Taifa letu.

    La msingi ni kuwa sawa tunasubiri hiyo Wings Of Kilimanjaro, Januari 2013

    Mdau
    DSM

    ReplyDelete
  6. bado nipo nipo sana..mh unatutega!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...