Mgeni
rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry
Mongi, akipanda mti wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji
hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni,
Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo,
akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya
upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni
Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni
Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30
kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa
wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
Meneja
wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi
wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni
hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta,
machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia
cha kampuni hiyo.
Naona wadau wamekataa kutandikiwa kanga ktk hii shughuli muhimu ya kupanda miti maana shurti ukubali kuwa karibu na nature yaani kukubali kugusa udongo.
ReplyDelete