Wizara ya Ujenzi inapenda
kutoa taarifa kwa Umma kwamba, Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dk. John Pombe
Magufuli (Mb) kwa Mujibu wa kifungu Na.3 (3), cha Sheria ya Usajili wa
Makandarasi namba 17 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2008, amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi. Uteuzi huu unafuata kumalizika kwa kipindi cha Bodi iliyotangulia
tarehe 30/11/2012. Katika uteuzi huu,
Waziri amemteua Eng. Consolatha Ngimbwa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi (CRB). Eng. Ngimbwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Electrics International Co. Ltd.
Wakati huohuo, Waziri wa
Ujenzi Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli (Mb) ameteua wajumbe nane (8) wa Bodi
ya Usajili wa Makandarasi kama
ifuatavyo:-
- Qs. Joseph Tango kutoka Tanzania Institute Quantity Surveyors
(TIQS). Kwa sasa Qs. Tango ni Makamu
Mwenyekiti wa TIQS.
- Eng.Samuel D. Shilla kutoka Association
of Consulting Engineers Tanzania
(ACET). Kwa sasa Eng. Shilla ni Mkurugenzi Mtendaji wa Service Consult Ltd.
- Eng. Lawrence Mwakyambiki kutoka Chama cha
Makandarasi Tanzania. Kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Wakandarasi na Mkurugenzi Mtendaji Mac
Contractors Ltd.
- Eng. Stephen P. Makigo kutoka Chama cha
Makandarasi Tanzania. Kwa sasa ni Mkurugenzi
Mkuu wa Manyanga Company Limited.
- Mr. Andrew Willson Masawe, akiwakilisha Sekta ya Biashara.
- Eng. Joseph M. Nyamhanga, Mkurugenzi wa Barabara,
Wizara ya Ujenzi.
- Mr. Abraham Senguji, Mkurugenzi wa Usuluhishi
na Upatanishi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
- Arch. Dudley B. Mawala, Mkurugenzi Mtendaji (Md Consultancy Limited). Anawakilisha Architectural Association of Tanzania (AAT).
Uteuzi
huu umefanyika tarehe 13/12/2012. Jukumu la msingi la Bodi ya Makandarasi ni
kusajili Makandarasi; kusimamia mwenendo wa Makandarasi; kujenga uwezo wa
Makandarasi wa Kitanzania na kulinda maslahi ya watumiaji wa Makandarasi.
Taarifa hii imetolewa na:
Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU


Hongera Eng. Consolatha Ngimbwa. Nakuomba kabla ya kumaliza muda wako huu, ujitahidi kwa udi na uvumba ku wezesha utaratibu wa kuwa na Quota >30% ya wanawake Engineers wenye uwezo kuteuliwa kuwa wajumbe katika Bodi ijayo.Wale uliyo wa mentor waje juu!
ReplyDelete