Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kukamilika kwa zoezi la kuwarejesha makwao wakimbizi wa Burundi waliokuwa kwenye kambi ya Mtabila Mkoani Kigoma, ambapo jumla ya wakimbizi 35,357 walirejeshwa hadi kufikia December 11 mwaka huu na kuifanya kambi hiyo kuwa bila ya wakimbizi.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi ya Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Judith Mtawali (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na na hatua mbalimbali zilizopitiwa hadi kukamilika kwa zoezi la kuwaondosha wakimbizi hao kukamilika.
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri huyo.

DECEMBER 11 mwaka huu zoezi la kuwarejesha kwao wakimbizi wa kambi ya Mtabila lilikamilika na kufanya idadi ya wakimbizi wote 35,357 kurejeshwa ispokuwa wakimbizi 1,540 tu ambao wako kwenye kambi ya Nyarugusu na hili ni kundi la 1993. 

Raia hao wa burundi awali8 walikua kwenye kambi ya Mtabila lakini kutokana na sababu mbalimbali walihamia kwenye kambi ya Nyarugusu ambayo wanaishi wakimbizi kutoka DRC bila ridhaa ya serikali na kusababisha kuvuliwa hadhi ya kuwa wakimbizi.

Tanzania hadi sasa inawakimbizi zaidi ya 60,000 kutoka nchini DRC, ambao inaendelea kuwahifadhi.
Kufungwa kwa kambi hiyo inafanya idadi ya kambi za wakimbizi zilizofungwa kufikia idadi ya Tisa ambapo kabla ya kufungwa kambi ya Mtabila kambi zilizofungwa ni pamoja na, Karago, Mtendeli, Kanembwa na Nduta (Kibondo) Muyovosi (Kasulu) Kitali (Biharamulo) Lukole (Ngara) na Mkungwa Kibondo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...