Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa kutoka kwa wadau wa afya wa Australia.
Muuguzi mkuu wa Idara ya Afya kutoka serikali ya Australia Bi. Catherine Stoddart (kushoto) akimkabidhi funguo za magari ya kubebea wagonjwa Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli katika viwanja vya wizara hiyo jijini Dar es salaam. Magari hayo 2 yaliyotolewa kwa msaada wa wadau wa afya wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Austaralia yatapelekwa kusaidia utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli(kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) funguo za magari mawili ya kubebea wagonjwa aliyokabidhiwa na wadau wa mashirika yasiyo ya serikali kutoka Austaralia.
Wawakilishi wa wadau wa afya mashirika yasiyo ya serikali kutoka Austaralia wakiongozwa na Muuguzi mkuu kutoka Idara ya Afya ya serikali ya Australia Magharibi Bi. Catherine Stoddart (wa pili kutoka kushoto waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada ya kukabidhi msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kabla hawajayataifisha.

    ReplyDelete
  2. kabla hayajapotelea njiani

    ReplyDelete
  3. pichani tu, yashataifishwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...