Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bwana Zahor Kassim Mohamed EL-KHAROUSY kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kusimamia
Uvuvi katika Bahari Kuu.
Taarifa
iliyotolewa na kutiwa saini na Ijumaa, Desemba 7, 2012 na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa uteuzi wa Bwana El Kharousy ulianza
Novemba 28, mwaka huu, 2012.
Kabla
ya uteuzi wake, Bwana Kharousy alikuwa Naibu
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Desemba, 2012
Ukisoma jina tu, unaweza kuuvaa mkenge na kufikiri jamaa ni mwarabu! shabaash, kumbe ni mpingo wa nguvu.
ReplyDelete