Tizi kali likiendelea wakati Simba wakijiandaa kwa mechi dhidi ya mabingwa wa Angola, C.R.Libolo kwenye mchezo wa awali na endapo watafuzu basi watakutana na El Merrikh ya Sudan kwenye hatua ya 16 bora hapo mwezi Machi 15, 16, 17.
Tizi likindelea
Kocha msaidizi Jamhuri Kihwelu Julio akisimamia tizi |
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharusi akiwa na Mwenyekiti wa Sunderland ya England, Ellis Short baada ya kukutana jana kwenye hoteli ya Hayat jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukutana, wawili hao walijadili kuhusiana na klabu hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibiashara pamoja na mafunzo na Simba imepata mwaliko.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Short alisema ushawishi wa Malkia wa Nyuki umechangia yeye kutoa mwaliko huo na anaamini timu zote zitafaidika.
"Mazungumzo yetu na Rahma yalikuwa mazuri sana, nimefarijika na ninaamini mwaliko niliotoa utakuwa mwanzo wa uhusiano mzuri kwa kuwa mwanamama huyu amenishawishi," alisema.
Malikia wa Nyuki ataiongoza Simba nchini England mwezi Machi ambako watatembelea viwanja vya Sunderland ikiwa ni pamoja na kujifunza uendeshaji wa klabu.
Awali Simba, ilijulikana kwa jina la Sunderland.
Habari na Picha zote na Saleh Ally
JAMANI WABONGO WENZETU KARIBUNI UK MSISAHAU KUJA PALACE KWA BIBI.MDAU ARTHUR STREET.
ReplyDeletewhat a name!
ReplyDeletewazo zuri kwa maadili ya soka.
ReplyDeleteJamani, hivi nyie viongozi wa Simba mtaacha lini kutufanya watoto sisi wanachama? Mnapenda sana kutoa evidence kwa kutumia picha. Nakumbuka katika mkutano wetu kule Police Mess pic Mwenyekiti Rage aliwahi kutuletea picha aliyopiga na Mbuyi Twite kama evidence kuwa tumemsajili. Wote ni mashahidi kuwa mchezaji huyu aliishia mikononi mwa watani zetu wenye akili. Sasa naona tunaoneshwa picha ya mama na huyu mzungu, ngoja tuone kama Simba itaenda Uingereza. Nina wasiwasi tutawaona watani zetu wakienda sisi tukiishia kuoneshwa picha za danganya toto
ReplyDelete