Ankal,
Kama nilivyokuambia mchana nimemfuatilia yule mtu aliyepiga simu chuo kusema ana vitu vyangu. Nimekuta ni kijana aliyemaliza form four anafanya kibarua Tanesco akingoja matokeo. Amaniomba msamaha sana kwa usumbufu nioupata kwani angetakiwa anitafute na kunirudishia mapema.
Kanirudishia wallet yangu na kila kitu isipokua fedha ambazo anasema wenzake walizigombania mara tu walipoiokota pale petrol station. Pia anasema alichelewa kunitafuta kwa sababu wenzake walimshawishi kuwa anaweza kujiingiza kwenye matatizo ya kudaiwa fedha nyingi iwapo angejitokeza na kusema kuwa ni yeye kaikota.
Kwa mara nyingine nikushukuru sana wewe na wengine wote walionisaidia kutangaza na kufuatilia upatikanaji wake. Mungu awabariki sana.
Mdau M. Mndeme

Safi sana wa tanzania tuwe na moyo huo.Mungu ambariki huyo KIJANA
ReplyDeleteJe ulimpa kitu kidogo?
ReplyDeleteUnaulizwa ulimdekshia dogo na kitu kidogo au ndo ukakoleza UPARE?
ReplyDeleteULIPASWA NA WEWE UTOE POSHO KAMA CHANGAMOTO NA MOTISHA KWANI PESA KITU GANI?
ReplyDeleteAma kwa hakika vijana kama huyo ni wachache sana. Tafadhalini tusiogope kurudisha vitu vya watu ulivyookota eti kwa kuogopa utadaiwa pesa. Kuwa MUUNGWANA. Hongera sana kijana
ReplyDeleteDah! nimeamini Mithupu ni zaidi ya gazeti, radio, na TV zote Bongo, yaani jamaa kibao wanasoma hapa, wenye uwezo na walala, hoi wote tupo pamoja, safii sana, Mithupu.
ReplyDelete