Ankal,
Kama nilivyokuambia mchana nimemfuatilia yule mtu aliyepiga simu chuo kusema ana vitu vyangu. Nimekuta ni kijana aliyemaliza form four anafanya kibarua Tanesco akingoja matokeo. Amaniomba msamaha sana kwa usumbufu nioupata kwani angetakiwa anitafute na kunirudishia mapema. 

Kanirudishia wallet yangu na kila kitu isipokua fedha ambazo anasema wenzake walizigombania mara tu walipoiokota pale petrol station. Pia anasema alichelewa kunitafuta kwa sababu wenzake walimshawishi kuwa anaweza kujiingiza kwenye matatizo ya kudaiwa fedha nyingi iwapo angejitokeza na kusema kuwa ni yeye kaikota.

 Kwa mara nyingine nikushukuru sana wewe na wengine wote walionisaidia kutangaza na kufuatilia upatikanaji wake. Mungu awabariki sana.


Mdau M. Mndeme

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Safi sana wa tanzania tuwe na moyo huo.Mungu ambariki huyo KIJANA

    ReplyDelete
  2. Je ulimpa kitu kidogo?

    ReplyDelete
  3. Unaulizwa ulimdekshia dogo na kitu kidogo au ndo ukakoleza UPARE?

    ReplyDelete
  4. ULIPASWA NA WEWE UTOE POSHO KAMA CHANGAMOTO NA MOTISHA KWANI PESA KITU GANI?

    ReplyDelete
  5. Ama kwa hakika vijana kama huyo ni wachache sana. Tafadhalini tusiogope kurudisha vitu vya watu ulivyookota eti kwa kuogopa utadaiwa pesa. Kuwa MUUNGWANA. Hongera sana kijana

    ReplyDelete
  6. Dah! nimeamini Mithupu ni zaidi ya gazeti, radio, na TV zote Bongo, yaani jamaa kibao wanasoma hapa, wenye uwezo na walala, hoi wote tupo pamoja, safii sana, Mithupu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...