Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana.
Picha ya Marehemu enzi za uhai wake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Prince David, mtoto wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, marehemu WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana.
Kutoka (kulia) ni Mume wa Marehemu, David Erasto Luharara, watoto wa marehem, Prince David na Abdulhaman David, wakiwa na huzuni.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu kuomboleza msiba huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jipeni moyo na poleni sana. Kazi ya Mungu.

    ReplyDelete
  2. Jamani nimeikumbuka hii sura ya huyu dada! Mume na watoto poleni sana kwa kuondokewa na mpendwa wenu Mungu awatie nguvu, na mumshukuru Mungu na msiwe na roho ya kisasi kwani sheria itafuata mkondo wake, kila binadamu amendikiwa siku na namna atakavyo ondoka hapa duniani. RIP Lokisa.

    ReplyDelete
  3. ...and she was a beauty,RIP.

    ReplyDelete
  4. Hii misafara mirefu na mwendo wa kasi wa magari ya viongozi lazima viangaliwe upya maana ni chanzo cha hatari kwa usalama wa raia wasio na hatia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...