KILIMANJARO RESTAURANT
COOKS -KITCHEN
SERVERS/WAIT STAFF-
BUSS BOY
DELIVERY DRIVERS
RESTAURANT SUPERVISOR
QUALIFICATIONS
UJUE KUONGEA KIINGEREZA/KISWAHILI
PIA UWE NA EXPERIENCE YA KAZI
NAFASI NI CHACHE WAHI MAPEMA
RESTAURANT ITAFUNGULIWA WIKI IJAYO MAENEO YA SILVER SPRING/WHEATON.
PIGA SIMU # 301-661-6207 KUANZIA 11AM-6PM
AU EMAIL - DMKPROMO@GMAIL.COM
hivi ni kuoneana tu na kuzidi kuingiza wafanyakazi wa kigeni nchini. Hivi kweli ni lazima kwa mpishi/cook kuwa anajua kiingilishi? jamani jamani wapeni kazi ndugu zetu wenye ujuzi na uzoefu wa kazi zao!
ReplyDeleteAnony wa kwanza: Nafikiri jamaa anzungumzia Silver Spring MD yaani Maryland huko US na sio hapa bongo.Hivyo sioni ni vipi ajira ya huko juu inaingiliana na kuongezeka wageni hapa bongo. Ila inayonitisha ni kuwa kweli kuna waongeao kiswahili huko ambao hawajui kiswahili? Najua pale Brighton Beach, Brooklyn, NY kuna generation ya warusi wasiojua kingereza ila sikutegemea kuwa na sie tuko hivyo. Labda ni mwambatano na matokeo ya Form Four? Blackmpingo
ReplyDeleteMabosi Kilimanjaro Restaurant:
ReplyDeleteMimi Msela nipo Bongo, je mnaweza kuniletea Makaratasi nami nije kufanya kazi huko Mgahawani Marekani kwa Obama?
Nina uzoefu wa vyakula vya Kizungu ambao niliupata nikifanya Kazi kwa Mzungu hapa Bongo na pia niliwahi kuwa Baharia nchi za Ulaya nikajua Kupika nikiwa Melini.
Hivyo ninamudu vyakula vya Kizungu adi vya asili kama hapa:
CONTINENTAL CUISINE:
-French rolls,
-Fries and toasts,
-Italian Sea Foods,
-Pastas and Pisas,
-Macaronis,
-Vanillas and Mochas,
-Cappucchinos and Lattes,
AFRICAN FOODS:
-Fufu(West African)
-Michemsho (Tanzanian)
-Mishikaki na nyama choma(Tanzanian)
-Makande,
-Ugali kwa mbaazi, michuzi ya nazi,
-Supu na Makongoro(Tanzanian)
Natuma C.V hiyo natanguliza Shukrani,
Ni mimi ndugu yenu Bozzen Diwakile,
Bongo, Daslaaam.
Mdau wa 3 ndugu Diwakile, wende Marekani na ukawe mwadilifu kwa nduguzo ktk Kazi utakayopewa na Udhamini utakaopata.
ReplyDeleteSio ufike huko tena utumie Ubaharia wako ukale kona ukazame huko Brighton Beach, brooklyn NY na Warusi (alikotaja Mdau wa Pili juu) badala ya kubaki kupika Hotelini ukarudi Melini!!!
Wewe Baharia Mpishi wa tatu (3) ni kweli utakuwa mwadilifu?, usije ukakanyaga kwa Obama ukageuka Mbogo ukaenda Brighton Beach, BROOKLYN-NY kwa Warusi anakotaja Mdau wa pili juu!
ReplyDeleteInaaminiwa ya kuwa ktk kazi hizi ni vigumu mtu kuziacha!
1.Uchimbaji Madini,
2.Uuzaji Gongo,
3.Upusha (Uuzaji Bange),
4.Uuzaji Mihadarati (Madawa),
5.Ubaharia,
Ukishaonja kazi hizo 5, mara zote utakwenda kazi zingine na unajikuta unarudi kazi hizo, ile Hata ukipewa Ukurugenzi wa Benki utaona haufai !!!
Duhhh ama kweli Mabahatia hawaaminiki!
ReplyDeleteMdau Bozzen Diwakile anaomba kazi kwa unyenyekevu lakini kazi puuu ndani ya UESI EI ohhh utamtaka !
Sio yule tena?
Baharia Diwakile kazi ya Upishi ataimudu vizuri sana kwa kuwa Mabaharia pia ni Wapishi wazuri.
ReplyDeleteLakini Baharia na Beach?, Beach la Marekani BROOKLYN-NEW YORK ?,hata huko Washington-DC atahama!!!, anaweza kuamua kukaa beach hata kama hatakuwa na kazi ya kufanya ili mradi anaziona Meli zinavyokata majui na kupiga honi za kuingia Bandarini na kuondoka (wanaita kupiga bunda) yeye Baharia Diwakile ataridhika !
Hawa jamaa wana Mzuka na midadi na beach sana mtakuwa mmemtega ni lazima ataondoka Hotelini atarudi Beach!!!
Kazi ni nzuri lakini ninajuta haipo hapa TZ ipo Majuu!
ReplyDeleteNitalazimika kuomba visa, tena visa zenyewe zinakuwa ngumu balaa, je mtanisaidiaje Mabosi?
ahahahahaha!
ReplyDeleteMdau Diwalile, Mpishi Baharia kazi itakuwa ngumu kwako!
Nadhani hapo utakapokuwa Kazini Jikoni pasiwepo na Bandari au Beach karibu ili usiweze kuona Meli zikikatiza.
Ni vile unaweza kuwa Jikoni ukachungulia dirishani ukaona Meli kubwa na ukasikia honi ya meli inapigwa (Poooooooliloooooooo!!!),
Ohhh hapo Diwakile mdadi wa Ubaharia utakupanda si utakuwa umeuwacha mchuzi unaungua ktk chungu Jikoni ukakimbilia Melini huko Beach?
Nafasi zimeisha aisee? Ka vp zikitokea tena tufahamishane aisee c lazima huko mbali hapa hapa tz kwetu, mambo ya hotel wng. Anna, arusha.
ReplyDelete