Wakazi wa wilaya Pangani wakimpokea kwa furaha na ngoma Mhe . Chiku Gallawa, mkuu wa mkoa wa Tanga katika moja ya mikutano ya hadhara wakati wa ziara yake ya siku tatu iliyokuwa na lengo la kusikiliza kero za wakazi wa pangani na kukagua miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa ( wa pili kutoka kushoto)akibadilishana mawazo na Kiongozi wa chama cha CUF baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika kata ya Madanga akisindikizwa na Mkuu wa Wilaya ya pangani Mhe. Hafsa .M. Mtasiwa ( wa pili kutoka kulia). Mradi huo unategemewa kuwahudumia wakazi wapatao 2500 wa kata hiyo.
Taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa ukuta wa bahari ikisomwa kwa mkuu wa mkoa na Engineer wa Wilaya Bw. Salum Bwaya wakati wa ziara yake. Wa nne kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa wilya ya Pangani Bw Rashid Neneka. Hata hivyo Mhe. Gallawa amewawajibisha watendaji ambao wanahusika moja kwa moja na utekelezaji wa mradi huo na kuhoji ubora wa ukuta huo ambao umekuwa na nyufa nyingi wakati bado ukiendelea kujengwa.
Ziara ya Mkuu wa mkoa Mhe Gallawa ilisimama kwa muda kuzima moto mkali uliowashwa na watu wasiojulikana katika hifadhi ya Ndorobo wilayani Pangani. Akiongoza uzimaji moto huo, Mkuu wa mkoa alikemea vikali vitendo vya uhalibifu wa mazingira ikiwemo uchomaji wa moto na pia ukataji wa miti ovyo.
Mkuu wa Mkoa alikitembelea kikundi cha seremala na uchongaji wa vinyago kinachoitwa “Upendo group” eneo la Kikokwe Bweni wilayani pangani. Mkuu wa mkoa aliongoza watendaji wengine kuunga mkono kikundi hicho kwa manunuzi ya bidhaa zao.
Team aliyoongozana nayo mkuu wa mkoa Mhe Chiku Gallawa ikijumuisha mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa wilaya ya pangani, Menyekiti wa Halmashauri ya pangani, viongozi wa vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama,wataalamu wa vitengo tofauti na watendaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...