Miss World Africa mwaka 2005 na Miss Tanzania mwaka huo huo,Nancy Sumari (pichani) jana alizindua Kitabu chake kiitwacho "Nyota Yako",ambacho ni Kitabu cha simulizi inayohadithia mafanikio na uwezo wa wanawake tofauti wa Kitanzania wanaoonyesha jitihada na upekee unaolenga kumhamasisha mtoto wa kike kwenye jamii kutaka kuota ndoto kubwa na kudhubutu kuyafanikisha yale ayawazayo.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitabu hiki cha Nyota Yako alikua Profesa Esther Mwaikambo, ambaye alikua mwanamke wa Tanzania kuwa daktari, muanzilishi wa MEWATA na rais wa chama cha wanasayanzi Tanzania. Prof Mwaikambo pia ni daktari wa watoto katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es salaam, na ni moja kati ya hadithi ya wanawake ambao hadithi zao zimesimuliwa kwenye kitabu.

Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Kitabu hicho imefanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na baadhi ya wageni maalum waliofanikiwa kufika katika hafla hiyo ya uzinduzi ambao ni pamoja na Faraja Kotta Nyalandu, Fina Mango, Jacqueline Ntuyabaliwe,Sophia Byanaku, Jokate Mwegelo, Shamim Mwasha, Khadija Mwanamboka, na wadau wa habari pamoja na marafiki.
Nancy Sumari (kushoto) akiwa na Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Profesa Esther Mwaikambo wakionyesha kitabu hicho mara baada yakukizindua.Kati kati ni Mtoto wa Nancy Sumari.
Nancy Sumari akisaini moja ya kitabu kabla ya kumpatia Mwanafunzi.
Nancy Sumari akiwa na Jacqueline Ntuyebaliwe (shoto) pamoja na Faraja Kotta wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamepewa vitabu hivyo.
Nancy Sumari na Jokate Mwegelo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Nancy. Keep it up

    ReplyDelete
  2. heh! huyo ndio professor? aisee! kikwete hebu mkumbuke huyu professor huenda akawa chachu ya tumethubutu na tunasonga mbele !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...