Eneo la tukio ambapo jengo la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa sita mchana leo maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha. Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa jicho la wasiwasi.
Rais Kikwete akiwa eneo la tukio tena leo, baada ya kutembelea jana, akitoa maagizo kwa Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova kwamba kila aliyehusika na ujenzi wa jengo hilo kuanzia mchoraji, msimamizi na mjenzi wahojiwe na wawajibishwe wakipatikana na kosa
Rais Kikwete akiongea na viongozi wa msikiti wa Shia ithnaasheri wakati anaondoka eneo la tukio
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa jana, Ijumaa, Machi 29, 2013, ametembelea jengo lililoporomoka na kusababisha vifo vya watu na majeruhi kwenye Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro mjini Dar es Salaam na amesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa yaliyotokana na kuporomoka kwa jengo hilo.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi wafiwa, anawapa pole nyingi walioumia na wanaoendelea kupatiwa matibabu baada ya kubanwa katika kifusi, wakiwamo watoto wadogo ambao walikuwa wanacheza chini ya jengo hilo la ghorofa 16 wakati lilipoporomoka asubuhi ya jana huku likiendelea kujengwa.
Rais Kikwete amewapongeza na kuwashukuru wananchi wote walioshiriki na wanaendelea kushiriki katika zoezi la uokoaji pamoja na vyombo na taasisi za umma na Serikali zinazoshiriki katika zoezi na kazi hiyo ya uokoaji.
Amewataka waendelee na jitihada hizo ili kama kuna watu ambao bado wamebanwa kwenye kifusi waweze kuokolewa ili wapatiwe matibabu, na kama watakuwa wamepoteza maisha basi miili yao ipatikane na iweze kupewa mazishi ya heshima yanayostahili mwanadamu.
Wakati alipotembelea eneo la tukio hilo, Rais Kikwete ametoa maelekezo mahsusi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Saidi Mecky Sadik pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova.
Rais amewataka kuhakikisha kuwa Mjenzi wa jengo hilo, Mhandisi Mshauri aliyekuwa anasimamia ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam ambaye alitoa kibali cha ujenzi na ndiye Mkaguzi wa ujenzi pamoja na mwenye Jengo wanapatikana haraka na kuwajibishwa ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete amezitaka taasisi za kitaaluma zinazohusina na shughuli za ujenzi – Wachoraji Majengo, Wakadiriaji Majengo, Wajenzi, Wakandarasi na Wahandisi nazo zichunguze tukio hilo kwa haraka na kwa karibu, ili zibaini yapi yalikuwa ni matatizo na zichukue hatua kwa mujibu madaraka na mamlaka ya taasisi hizo kwa sababu zinayo madaraka na mamlaka hayo.
Rais pia amesema kuwa wakati umefika kwa taasisi hizo sasa kujihusisha kwa karibu zaidi na matatizo yanayojitokeza katika shughuli za ujenzi kwa sababu kila yanapoporoka majengo inakuwa heshima mbaya kwa taasisi hizo.
Hivyo ni muhimu kwa taasisi hizo kufanya uchunguzi wa kubaini nini chanzo cha kila tukio kuanzia na lile la jana – kama ilikuwa ni udhaifu katika uchoraji, kama ilikuwa ni udhaifu katika ukandarasi, kama ilikuwa udhaifu na Ushauri ili hatua stahiki zichukuliwe.
hilo jengo la kulia linasubiri kazi imalizike na lenyewe lianguke kwani kwa kuliangalia tu na mcho haya yangu yenye ukungu wa glaukoma bado naliona limekaa bega moja ushauri wangu walibomowe kabla hatujapata maafa mengine.
ReplyDeletesiku hizi hapa dar kuna vyuo vya ukandarasi vya usiku usiku pia vile vya mitandaoni ndio usiseme sasa hivi vikwangua anga tunavyojidai navyo sasa vinatusalimia migongoni na kutufunika tukiwa hai.
mungu tusaidie baba yangu eeee.
mdau kariakoo.
Ukiangalia picha ya kwanza after yoube video, ilo jengo refu lililobakia wala haliendani na size ya iyo plot. Hyo ni maeneo sio ya ku-accomodate vikwangua hanga. Ni maeneo ya kuaccomodate ghorofa sizisozidi sita. Tuna mipango miji without vision.
ReplyDeleteKwanza hilo jengo linalojengwa hata mie mwenye macho mabovu naona limepinda. Wanajali mali kuliko utu wa mtu. Very sad. Poleni sana wafiwa.
ReplyDeletecamera tu ya michuzi na bird eye yake jengo lipo sawa ila ni feki na pia saruji feki,hiki kifusi hatoki mtu na tulivokuwa hatusign fire book tumeumia
ReplyDeleteHaya magorofa mengi ya Bongo ni time bomb
ReplyDeleteleo baada ya kumuona jinsi mh rais wangu kikwete anavyoongea ndio hakika nimegundua kuwa ni mtu mwema sana kuliko watu wanavyomsema...rais kikwete ni mtu mpole na mwenye huruma...asante Mungu kwa kutupa rais mwema...pia nimegundua watendaji wake (kwa jinsi wanavyoongea kwenye hii clip) si watu wema...nadhani kwa watu waliosoma body language watanielewa vizuri...kuwa rais wa watu wa namna hii ni mzigo mkubwa sana..pole sana mh rais kikwete maana matatizo ya wa-tz yamekuelemea badala ya kutatuliwa na watendaji.
ReplyDeleteBwana Mungu nakuomba uendelee kumtunza na kumpa afya njema mh rais kikwete...damu ya Bwana Yesu ikufunike mh rais popote uendako na Mungu azidi kukutangulia daima. AMEN
mdau
sweden
Hizo ghorofa zenu huenda nisizipande maana zisije kuanguka nikiwa ndani yake nikirudi.
ReplyDeleteHuyu mkandarasi ndiyo kati ya wale waliofaulu form four. Sasa wale waliofeli watakapokuwa makandarasi serikali itapiga marufuku kuegamia au kupuliza majengo wanayojenga.
ReplyDeleteLile jengo la lililoporomoka la Keko na la Kisutu liliundiwa TUME na Mheshimiwa Lowasa na hatujui yaliyojiri. Pili majengo mengi yamejengwa gorofa za nyingi kwenda juu bila kujali ngazi za dharura za pembeni(side steps) emergency exits(milango ya dharura ikitokea ajali ya moto, ujenzi ambao pia hauzingatii kwa ujumla dharura ikiwemo kuwemo maduka safu ya chini ilimradi juu ghorofani ni makazi ya watu! what hell! CRB mmko wapi, nyie NHC ambao mna ubia na hawa wamiliki mko makini; ndio public private partnership?
ReplyDeleteMheshimiwa JK nguruma.
JK WEWE NA WENZIO MNAZUNGUKA UKWELI TATIZO NI RUSHWA. RUSHWA NI KAMA MCHWA, INAKULA NDANI KWA NDANI. HATA TUKIWA NA SHERIA MAHSUSI, HATA TUKIWA NA WATENDAJI MAHSUSI, RUSHWA IKIISHA INGIA MAMBO MENGI HUPINDWA. INASIKITISHA NA INASIKITISHA SANA.....KAMA ILIVYO DAWA YA MCHWA , DAWA YA HAYA TUNAYOTAONA NI KU-ERADICATE RUSHWA JK. REST IN PEACE WALE WALIOPOTEZA MAISHA YAO....NAAM KWA HALI HII WENGI TUTAFUATA
ReplyDelete