Jumla ya maiti 18 zimeopolewa katika kifusi cha jengo la ghorofa zaidi ya kumi lililopromoka jana asubuhi katika mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam, idadi hiyo ya watu waliopoteza maisha ikiwa ni ya kihistoria kwa majanga ya aina hii.

Mwili mmoja umeopolewa muda mfupi uliopita, ikiwa ni masaa kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik kuthibitisha mapema asubuhi kwamba miili 17 ilikuwa imepatikana baada ya kazi za uokoaji ya usiku kucha na inayoendelea hivi sasa.

Makampuni kadhaa ya ujenzi yamejiunga katika zoezi hilo toka usiku kusaidia kuinua vifusi na kuopoa miili ya marehemu. Uwezekano wa kukuta mtu aliye hai hadi sasa ni mdogo sana wakati waokoaji wakiwa ni pamoja ya wanajeshi na vijana wa JKT wakiendelea na kazi.

Tutaendelea kuwapa Updates kila itapobidi.

Mola aziweke roho za marehemu mahala pema peponi - AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inna lillah wa inna ilayhi rajiun

    ReplyDelete
  2. Ifike wakat roho za watu ziwe na thaman kuliko pesa... Tutapoteza wangapi kwa ajili ya uzembe na uchu wa pesa wa watu wachache... Tucsubiri watu wapotez maish ndo hatua zichukuliwe, hebu hatua zichukuliw kbl roho ziczo na hatia hazijapotea.. Ili likitokea janga ionekane ni bahati mbaya kwel.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...