Wafanyabiashara wa kitimoto mjini Iringa wakionyesha milango yao iliyofungwa na mgambo leo kama njia ya kupinga uuzaji wa nyama ya nguruwe (kitimoto)
Hapa wakiamua kuchimba barabara kuzuia magari kupita eneo hilo
Maandamano ya kupinga marufuku ya uuzaji wa kitimoto leo
Na Francis Godwin
Wafanyabiashara wa kitimoto katika eneo la vibanda vya UVCCM mjini Iringa leo wamewatimua mgambo wa Manispaa ya Iringa ambao wamefika eneo hilo kufunga biashara zao kama njia ya kunusuru wananchi na ugonjwa wa homa ya nguruwe.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 12 jioni baada ya ofisa mifungo Manispaa ya Iringa akiwa na mgambo kufika eneo hilo kufunga biashara zote za kitimoto eneo hilo.
Wakizungumzia hatua hiyo wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanashangazwa na uamuzi huo wa uongozi wa afya Manispaa ya iringa kuwazuia wao kufanyabiashara hiyo wakati maeneo mbali mbali maarufu nyama hiyo ikiendelea kuuzwa kama kawaida .
Hivyo wameutaka uongozi wa Manispaa ya Iringa kusitisha mpango huo kwani unawatesa wananchi hao wajasiriamali wenye kipato cha chini ambao wanategemea biashara hiyo.
katika hatua nyingine wafanyabishara hao na wateja wao wamewatimua mgambo hao na ofisa mifugo huyo katika eneo hilo kwa madai muda waliokuwa wakifanya kazi ni muda ambao si wa kazi na kudai kuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa .
wacheni kula wanyama wenye magonjwa hao mbona hamsikii wenzenu huku ughaibuni wanaongoza kwa magonjwa mbali mbali yakiwemo kansa kwa kula kiti moto.
ReplyDeleteAnony wa Kwanza, unaongea ujinga mtupu. Kila mnyama ana hatari ya kumpa binadamu ugonjwa kwa kumwambukiza. Ng'ombe anaweza kuzuru binadamu kwa kumpa ugonjwa (mad cow disease) na pia kuku (samlonella). Nguruwe anaambukiza mafuwa (Influenza).
ReplyDeleteMdau wa kwanza anasema kuwa ughaibuni unaongoza magonjwa mbalimbali lakini amesahau kusema kuwa wana tiba thati ya magonjwa na wananchi wao wanaishi miaka 80 wakati Watanzania wanakufa miaka 52kwa kukosa madawa, tiba bora na hali safi ya mazingira (angalia picha za mwanzo za leo sinaonyesha maji machafu yanaotoka chooni katika mitaa yetu).
Na kama kiti moto ni sababu ya magonjwa ya kansa, basi wachina na wasia wengi wangekufa zaidi kwa kuwa ni chakula chao muhimu kila siku. Utakuta wao ndio wanaishi maisha bora na marefu kuliko sisi na sababu ya vurugu hapo Iringa ni kwa wananchi kukosa elimu ya kujua madhara ya ugonjwa ambao unaweza kutokea nchi yoyote ile. Elimu ni muhimu hapo. Kama huelewi sayansi, utaelimishwa vipi kijijini?
Hivi Meya wa manispaa ya Iringa ni dini gani?
ReplyDeleteMchangiaji wa pili hapo juu, soma Deuteronomy 14 : 8 kwenye biblia yako, Biblia yako yenyewe inakukataza usile hiyo nyama ya nguruwe,ni chafu !!!. Why eating something that was made purposely to take care the Cabbage ?!!!, you must be very foolish !!!. Usibishane na maandiko !!!,tatizo lenu hamsomi wenyewe vizuri maandiko yenu bali mnawaachia watu wachache msomewe !!!,you are very Sad !!!
ReplyDeleteHiii kali yaani nimechekaje mpakaa!!! hapo chacha. sema na kiti moto. wanachi urohoo wote umewatoka, atawakiambiwa hawasikii, kazi kweli kweli, mpaka wamewatimua mgambo wote na dr. Mifugo shughuli pevu ilikuwa, na hii yote ni kutokana na umasikini, wanambiwa hatari wao bado wapo kimasirahi zaidi, lakini siyo kiafya
ReplyDeleteEat wateva you can to survive ila usile mtu tuh
ReplyDelete