Wafanyabiashara  wa kitimoto  mjini Iringa  wakionyesha  milango yao  iliyofungwa na mgambo  leo kama njia ya kupinga  uuzaji  wa nyama ya nguruwe (kitimoto)
 Hapa wakiamua  kuchimba barabara  kuzuia  magari kupita eneo hilo 
 Maandamano ya  kupinga  marufuku ya uuzaji  wa kitimoto leo 
 

Na Francis Godwin
Wafanyabiashara  wa  kitimoto katika  eneo la vibanda  vya UVCCM mjini  Iringa  leo wamewatimua mgambo  wa Manispaa ya Iringa ambao  wamefika eneo hilo kufunga biashara  zao kama  njia ya kunusuru wananchi na ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Tukio hilo  limetokea leo  majira  ya  saa 12 jioni baada ya  ofisa mifungo  Manispaa ya Iringa  akiwa na mgambo kufika   eneo hilo  kufunga   biashara  zote za kitimoto eneo hilo.

Wakizungumzia hatua  hiyo  wafanyabiashara  hao  wamesema  kuwa wanashangazwa na uamuzi huo  wa  uongozi  wa afya Manispaa ya iringa  kuwazuia  wao kufanyabiashara  hiyo  wakati maeneo mbali mbali maarufu  nyama  hiyo ikiendelea  kuuzwa kama kawaida .

Hivyo  wameutaka  uongozi  wa Manispaa ya  Iringa  kusitisha mpango huo  kwani  unawatesa wananchi hao  wajasiriamali  wenye kipato cha chini ambao  wanategemea biashara  hiyo.

katika hatua nyingine  wafanyabishara  hao  na  wateja  wao  wamewatimua  mgambo hao na ofisa mifugo  huyo katika  eneo hilo kwa madai  muda  waliokuwa wakifanya kazi ni muda ambao si wa kazi na  kudai kuwa  wanatumiwa na  wafanyabiashara wakubwa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. wacheni kula wanyama wenye magonjwa hao mbona hamsikii wenzenu huku ughaibuni wanaongoza kwa magonjwa mbali mbali yakiwemo kansa kwa kula kiti moto.

    ReplyDelete
  2. Anony wa Kwanza, unaongea ujinga mtupu. Kila mnyama ana hatari ya kumpa binadamu ugonjwa kwa kumwambukiza. Ng'ombe anaweza kuzuru binadamu kwa kumpa ugonjwa (mad cow disease) na pia kuku (samlonella). Nguruwe anaambukiza mafuwa (Influenza).

    Mdau wa kwanza anasema kuwa ughaibuni unaongoza magonjwa mbalimbali lakini amesahau kusema kuwa wana tiba thati ya magonjwa na wananchi wao wanaishi miaka 80 wakati Watanzania wanakufa miaka 52kwa kukosa madawa, tiba bora na hali safi ya mazingira (angalia picha za mwanzo za leo sinaonyesha maji machafu yanaotoka chooni katika mitaa yetu).

    Na kama kiti moto ni sababu ya magonjwa ya kansa, basi wachina na wasia wengi wangekufa zaidi kwa kuwa ni chakula chao muhimu kila siku. Utakuta wao ndio wanaishi maisha bora na marefu kuliko sisi na sababu ya vurugu hapo Iringa ni kwa wananchi kukosa elimu ya kujua madhara ya ugonjwa ambao unaweza kutokea nchi yoyote ile. Elimu ni muhimu hapo. Kama huelewi sayansi, utaelimishwa vipi kijijini?

    ReplyDelete
  3. Hivi Meya wa manispaa ya Iringa ni dini gani?

    ReplyDelete
  4. Mchangiaji wa pili hapo juu, soma Deuteronomy 14 : 8 kwenye biblia yako, Biblia yako yenyewe inakukataza usile hiyo nyama ya nguruwe,ni chafu !!!. Why eating something that was made purposely to take care the Cabbage ?!!!, you must be very foolish !!!. Usibishane na maandiko !!!,tatizo lenu hamsomi wenyewe vizuri maandiko yenu bali mnawaachia watu wachache msomewe !!!,you are very Sad !!!

    ReplyDelete
  5. Hiii kali yaani nimechekaje mpakaa!!! hapo chacha. sema na kiti moto. wanachi urohoo wote umewatoka, atawakiambiwa hawasikii, kazi kweli kweli, mpaka wamewatimua mgambo wote na dr. Mifugo shughuli pevu ilikuwa, na hii yote ni kutokana na umasikini, wanambiwa hatari wao bado wapo kimasirahi zaidi, lakini siyo kiafya

    ReplyDelete
  6. Eat wateva you can to survive ila usile mtu tuh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...