Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mkwakyembe(mwenye tai nyekundu), akiangalia
mataruma 35 yaliyoibiwa kutoka katika stesheni ya Reli ya Pugu na kusafirishwa
kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuja kuuzwa kama chuma chakavu . Kulia kwa
Waziri wa Uchukuzi ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa
tai ya mistari).
Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba akipata maelezo na mataruma yaliyobiwa
kutoka kwa ACP Saada Haji ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi Cha Polisi Reli, wakati
walifanya ziara ya kuangalia mataruma ya reli yalyibiwa katika vipindi tofauti
tofauti yaliyopo katika eneo la Mivinjeni kurasini. (Picha
na kitengo cha mawasiliano Serikalini Uchukuzi).
Shehena ya mataruma ya
zaidi ya Tani 15 yaliyokamatwa na askari wa kikosi cha reli yakiwa katika eneo
la reli Mivinjeni baada ya kukamatwa tarehe 14/2/2013 na dreva wa Lori hilo
kukimbia. Waziri wa Uchukuzi na Naibu Waziri wamefanya Ziara katika eneno hilo leo
kujionea mzigo wa Mataruma yaliyobiwa katika vipindi tofauti tofauti.
Waziri
wa Uchukuzi.Dkt Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu),akipata maelezo kutoka
kwa ACP Saada Haji Mkuu wa kikosi cha Polisi (Reli)(aliyevaa hijabu) ya namna
wezi wa Mataruma hayo walivyoiba na kukamatwa na askari wake tarehe 14 Februari
2013. Kulia kwa ACP Saada Haji, ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt
Charles Tizeba.
Magunia
yaliyotumika kufunikia mataruma ya Reli ambayo yaliibiwa na kusafirishwa
kutokea Tabora tarehe 14/2/2012 na kubebwa kwenye Lori la Mizigo la Kampuni ya Unga
ya Azania (linaloonekana mbele) kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuuza kama
chuma chakavu. Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Uchukuzi,
Dkt. Charles Tizeba wamefanya ziara ya kuangalia mataruma hayo leo mchana
jijini Dar es Salaam. Mataruma hayo yamehifadhiwa katika yadi ya Reli iliyoko
Mivinjeni Kurasini, Dar es Salaam.
wanaoiba mataruma ni wale wenye magari makubwa kisa reli inaharibu biashara
ReplyDeleteHaya malori yapigwe fine kubwa, kama 50,000,000. iwe mfano kwa wengine
ReplyDeleteDereva amekimbia, je na Lori pia amekimbia nalo?
ReplyDeleteKilichopo ni kulikamata Lori na mmiliki akatafutwa na kumtaja Dereva wake!