SAKATA la serikali kuikataa katiba ya TFF imechukua sura mpya baada ya katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah kumtaka Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amos Makala kujiweka pembeni na kuacha kuzungumzia masuala ya uchaguzi wa shirikisho hilo.

Angetile aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa Makala alishaonyesha kuwa ana upande anaoupendelea ndio maana alitoa maoni yake kama mdau alipokuwa jimboni kwake Mvomero na alipofika Morogoro mjini akadai lazima Serikali itoe tamko zito.

"Katika suala hili tunamuomba Makala akae mbali ameshaonyesha interest, Waziri (Dk Fenela Mukangara) bado tunaimani naye, tumeomba kikao kifanyike kesho kutwa (kesho) Alhamis na kama itashindikana basi kifanyike baada ya tarehe 13 kwa kuwa hapa katikati kuna vikao vya CAF (Shirikisho la Soka Barani Afrika).

"Serikali sio Wizara peke yake ni pamoja na sisi kwa hiyo ikitoa maagizo itoe yanayotekelezeka sio maelekezo ambayo ni vigumu kutekelezeka."alisema Osiah ambaye pia aliwataka waliopoteza sifa za kuingia TFF kuacha kuongea ongea ovyo kwenye vyombo vya habari kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mpira hali kadhalika kwa waliofungua kesi Mahakamani kupinga mchakato wa uchaguzi.

Akizungumzia kauli hiyo ya Angetile, Makala alisema anaheshimu kauli iliyotolewa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga wiki iliyopita ya kuomba kukutana na Waziri kujadili suala hilo lifike mwisho na kudai kuwa kauli ya katibu huyo wa TFF ni yake binafsi na si msimamo wa shirikisho.

" Angetile anaupande ndio maana mimi nilipotoa maoni yangu kama mdau ilimuathiri yeye na mgombea wake, niliwaudhi, alafu hawezi kusema nikae pembeni wakati michezo ni eneo langu katika kazi, wapende wasipende suala lao mimi ndio ninayelisimamia.

Mapema mwezi uliopita kamati ya rufaa chini ya Idd Mtiginjola ilimuengua mgombea wa nafasi ya urais Jamali Malinzi kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 kwa madai ya kukosa uzoefu, na Naibu Waziri Amos Makala alikaririwa akitoa maoni kama mdau wa michezo alisema ameshtushwa kwa Malinzi kuenguliwa na kudai kamati ya rufaa imenunua dharua kwa gharama ndogo.

"Bila kupepesa macho wala kuumauma maneno, nikiwa mdau wa soka na kuuvua wadhifa wangu wa unaibu waziri, hapa kuna tatizo kwani kamati haijamtendea haki Malinzi," alikaririwa Makalla.

Hata hivyo jana alisisitiza: "Kwa taarifa yao Waziri kasafiri kwa siku 10 nina maelekezo yote ya suala lao hivyo waje nilishasema milango ipo wazi, wasichague nesi wakati wapo leba, kwanza aliyefikisha suala hili kwenye matatizo ni Angetile mwenyewe baada ya kufanya makosa yake ya kiutendaji nilidhani angekaa kimya na kutafakari makosa aliyofanya badala ya kuongea ongea."alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Je, TFF mpo msituni au mpo kwenye nchi yenye Serikali?

    Ninyi Makundi ya pande mbili TFF ndio mkae pembeni muiache Serikali iunde sera ya Michezo nchini na ifanye kazi yake.

    Makundi ya PANDE MBILI ndani ya TFF woooote mmeoza na hamna sifa za Uongozi ukiwemo wewe unaetoa Mashariti kwa Serikali wewe Angetile Osiah.

    Tunataka Serikali iingilie kati suala hili, licha ya kuwa kuna Demokrasia zenu za FIFA lakini kwa kuwa Mpira ni zaidi ya Burudani kwa vile mpira ni:

    -Uchumi,
    -Biashara,
    -Diplomasia/Mahusiano ya Mataifa,
    -Ustawi wa Jamii na Afya,
    -Ajira,

    Kwa hayo matano (5) hatuwezi kumkabidhi Fisi Bucha la nyama, lazima tulihami Bucha hilo!!!

    ReplyDelete
  2. IF NO TFF = NO FOOTBALL,THEN,NO FOOTBALL=NO TFF(TRUE or FALSE?)

    Tuache utani lakini alivyosema mdau wa kwanza hapo jjuu, wewe Angetile hiyo jeuri ya kutoiheshimu serikali unaitoa wapi?

    David V

    ReplyDelete
  3. FIFA kuweka taratibu za kutoingiliwa ni baada ya kuona ambavyo serikali zilikuwa zikiharibu soka hata hapa kwetu tuliona. Tenga na wenzake wametutoa mbali na kutufikisha mahali ambapo tunakaribia ku-take off!msikilize Tenga anapoongea facts anazotoa ni za uhakika he's a Leader. Upande wa serikali unatufedhehesha umeingilia mambo na kukaa upande mmoja wa kutetea wagombea wasiostahili kulingana na taratibu, hawana points za kutosha kama alizotoa Tenga,inasikitisha kuona watu wachache wanayumbisha nchi katika sekta hii ya soka.Halafu kuwa mdau wa soka sio lazima uwe kiongozi TFF hawa watu wanatia aibu wanang'ang'ania sana TFF miaka yote, walishapewa nafasi wakavuruga,unaweza anzisha timu ukakuza vipaji hapo utakuwa umelisaidia Taifa sio lazima uwe kiongozi TFF, au kuna vitu wanavyofuata?

    ReplyDelete
  4. Acheni upumbavu wenu akina Angetile na Genge lenu la Kamari ya Karata Tatu.

    Michezo ni kwa Maslahi na Ustawi wa nchi na sio genge la watu wachache!

    Hii ni nchi, na pia mkumbuke ya kuwa hatuwezi kuendesha mambo kienyeji kwa manufaa ya genge la watu wachache kwa faida ya nani?

    ReplyDelete
  5. Msifikiri mtaishi kwa kutegemea mgongo wa FIFA na kukingiwa kifua na FIFA mnaweza kujikuta Serikali itatoa maamuzi mazito na hata kujitoa kwenye Uanachama wa hiyo FIFA yenu!

    Sijui mtafanya nini hapo?

    ReplyDelete
  6. Angetile Osiah na Magenge ya ndani ya TFF ni muda wa kunoa mapanga na majembe mjiandae kwa Kilimo!

    Ni kwa nini?

    Ni vile Saccos(TFF) mliyokuwa mnaitegemea miaka kwa miaka na mliyoweka matumaini mtafikia malengo mengi kimaisha, ni kuwa Saccos(TFF) imefilisika kwa kuwa Mweka Hazina ametoroka na funguo za Ofisi!!!, hadi sasa hajulikani alipo.

    Hivyo haijulikani kama Akiba ya Mfuko ipo ndani au ametoroka nayo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...