Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano kukutana na Watanzania waishio Newcastle nchini humo.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe akihutubia watanzania waishio mji wa Newcastle jana. Katika hituba yake Balozi Kallaghe aliwasifu Watanzania wenye kuwa na jumuiya zao mahali walipo, akisisitiza hiyo ndiyo mojawapo ya njia kuu za kudumisha umoja, upendo na amani miongoni mwa Watanzania waliopo ughaibuni.
  Juu na chini Balozi Peter Kallaghe akipozi na baadhi ya wadau wa Newcastle baada ya kukutana nao jana mjini humo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. sielewi kazi za mabolozi wa Bongo siku hizi, hivi ni kuangalia masilahi ya economic refugees? Hebu nielezeni job description yao mpya.

    ReplyDelete
  2. hivi ana uhakika hawa ni watanzania au wasomali na waburundi?

    ReplyDelete
  3. Wacheni pumba nyie wadau wa #1&2.

    Kwa hiyo hao jamaa zetu wanaonekana kama wakimbizi au Wasomoli kweli? Wacheni kuongea upuuzi. Kama wivu umewajaa kwa vile ukufanikiwa kupata visa siyo kisa cha kuwakandia ndugu zenu. Kila mtu na bahati yake, jaribu yako na wewe. Kazi ya Balozi ni nini?!! Mie nadhani kuangalia maslai ya Watanzania huko waliko. Jamaa wengine mna chuki binafsi mpaka mnaota pembe(kweli hayafichiki hayo). Michuzi naomba usibanie nifikishie meseji.

    ReplyDelete
  4. hakujua anatembelea wasomali,na wanyarwanda,waburundi,wasomali.hapo ukiuliza vitambulisho angejikuta mtanzania peke yake.poor kalaghe

    ReplyDelete
  5. majungu majungu majungu... thats why we are still behind

    ReplyDelete
  6. This is my hometown Newcastle and you are all very welcome to come visit me in Newcastle. HAHAHA also jealousy is a disease so get well soon darling ;).

    ReplyDelete
  7. HAHAH jealousy is a disease get well soon darling also you are welcome to come visit me in my Home town of Newcastle.

    ReplyDelete
  8. Wawe wasomali ,warundi,wanyarwanda au wakongo siyo tataizo maisha popote na bora maisha yao yanawaendea vizuri,na pesa ikipatikana inakwenda bongo ,kujenga bongo ,ukinunua gari linaenda bongo siyo somalia wala sijui wapi!,ushauri wangu wabongo pigeni miguu yote ili mradi usifanye uharifu anayepiga MDOMO wala asiwashughulishe bora yenu yanawaendea
    siku njema mdau Dar Magomeni

    ReplyDelete
  9. NAFIKIRI NYIE WOTE MNAOWAPONDA HAO NDUGU ZETU UPEO WENU NI MDOGO SANA KATIKA DUNIA YA SASA.
    YESU MWANA WA MUNGU NA WAZAZI WAKE WALIKUWA WAKIMBIZI HAPO ZAMANI ZA KALE KABLA HATA BABU WA BABU YAKO NA VIZAZI VYENU HAVIJATOKEA. VIONGOZI WOTE WAKIPINDULIWA WANAZIKIMBIA NCHI ZAO NA KUOMBA HIFADHI ZA KISIASA NA WANAPEWA ULINZI NYUMBA NA KULIPWA PESA NYINGI TU! HUKU KATIKA NCHI WALIZOTOKA WAKIWA WAMESHAIBA SANA! NA BADO WANAHESHIMIWA MPAKA LEO KULE WANAPOKIMBILIA!
    MTU ASIE KIONGOZI AKIOMBA UKIMBIZI KUNA DHAMBI GANI KWAKE? KWANI WAO NDIO WALIOANZISHA JAMBO HILI?
    MBONA KUNA VIONGOZI WALIKAA ZAIDI YA MIAKA 30 MADARAKANI LEO HII WAO NA WATOTO WAO WOTE WAMEKUWA WAKIMBIZI? MAISHA NI POPOTE NA DUNIA HAINA MWENYEWE. KIKUBWA NI AKILI YAKO ILI UWEZE KUISHI MAISHA SAWA KAMA WATU WENGINE. NINA MARAFIKI ZANGU WAWILI WALIKUWA VIBAKA HATARI SANA HAPO BONGO! LEO HII WAPO HUKU WANAISHI MAISHA MAZURI SANA NA WAMEJIFUNZA KAZI AMBAYO INAWASAIDIA POPOTE PALE WATAKAPOAMUA KUISHI!
    HUKU MTU YOYOTE UNASOMESHWA TENA BURE ILI UWEZE KUJITEGEMEA. LEO HII VIBAKA WALE WA ZAMANI WANASAIDIA SANA NDUGU ZAO NA WATU WENGINE WENGI TU! ILA WANGEKUWA HAPO BONGO SIKU NYINGI TUNGEWASAHAU MANA MMOJA ALIWAHI KUVISHWA TAIRI LA MOTO AKAOKOLEWA NA POLISI KABLA HALIJAWASHWA!
    NIMEKUPA MFANO ILI UJUE MAISHA JINSI YALIVYO.
    KARIBU SANA NA WEWE UJE UONE RAHA YA HUKU NA JINSI WATU WOTE WANAVYOISHI MAISHA SAWA YA KUFANANA KWA KILA KITU.

    ReplyDelete
  10. Mdau NewcastleApril 23, 2013

    Wadau wa # 1,2 and 4. Mnaoenekana nyie ni wafu wa kimawazo. Mosi,Madai yenu hayana Uthibitisho na kama mnajiaamini weekni majina yenu halisi ili tongee pasi kumumunya.

    Balozi kama mwakilishi wa watanzania wote anawajibu wa kuwatembelea watanzania wote bila ubaguzi.Kama una tatizo na hili, kajinyonge.

    Tatizo letu kubwa watanzania hatupendi kuungana mkono katika kujenga mambo ya msingi. Mda ambao umeutumia kuandika utumbo hapo juu, ungeutumia kuuliza ni namna gani unaweza kuungana na watanzania wa Newcastle ili kuboresha nyanja mojawapo ya kiuchumi/kisisa Tanzania ungekuwa umeleta tija kwa Taifa.

    Lakini zaidi ya yote, Maelezo yenu yanaonesha Tanzania ina safari ndefu kuelekea kwenye mageuzi ya fikra, ili tuweze kufika tunapotaka kufika.

    ReplyDelete
  11. WABNGO KWA ROHO ZA KOROSHO, DUH!!! MARA WANYARWANDA, WASOMALIA.NYIE NDIO WALEWALE WA SIZITAKI MBICHI HIZI. HA HA HA HAAAAAAAAA!

    ReplyDelete
  12. Am a boy of a 15 i came to Newcastle at the age of 3 just imagine you may aswell class me as English my sister is swahillli and she is going to Nothumbria University ? people are you not proud ?

    ReplyDelete
  13. SINA WIVU2013April 23, 2013

    KWA.BALOZI KALAGE HONGERA SANA KUWAJALI WATANZANIA, NAJUA WEWE NI MWANADIPLOMASIA NA ZIMETIMIA TIMAMU, USITETEREKE NA WENYE BONGO LALA. KWA WANA NEWCASTLE HONGERENI KUMPA HESHMA BALOZI WENU, MSIWASIKILIZE WANABONGO LALA, KUWENI VYOVYOTE VILE NINYI NI WATANZANIA DEAL NA FAMILY ZENU MJENGE TAIFA LENU TANZANIA MRADI HAMVUNJI SHERIA ZA NCHI MLIOPO,HAO WASEMOA HOVYO SI LOLOTE SI CHOCHOTE ZAIDI YA WIVU KWAMBA HUO UKIMBIZI WANOUSEMA WAMEUKOSA NA HAWATOUPATA, WIVUUUUUUUUU TU. NAWATAKIA KILA LA KHERI SOMESHENI WATOTO WENU, BEBENI ZIGO MJENGE TAIFA LENU.KULENI MIKUKU YA QUEEN. WAO WAMEKULA VINGAPI VYA KWETU? NA KWA TAARIFA YAO HAO WENYE WIVU NI KUWA HATA BONGO KUNA WAKIMBIZI TELE TOKA KILA NCHI HAPA DUNIANI CHA AJABU NINI? KEEP UP WANANEWCASTLE NAWABONGO MLIO UK.

    ReplyDelete
  14. I salute you(boy of 15), hope you will follow your sister's footsteps. God bless you boy. and shame on all who wrote negative comments above.

    ReplyDelete
  15. INTERESTING INDEED. WATU HAO HAO MNAOWAPONDA NDIO MUWAOMBAO DOLA WAKIJA BONGO. REMEMBER, WANAILETEA NCH FOREIGN CURRENCY PIA. SASA WEWE PIGA MAJUNGU TU BILA KUFIKIRI. KAMA HUTAKI PANDA JUU UKAZIBE.
    NOT BECAUSE SOMEONE IS NOT LIVING IN BONGO DOES NOT MEAN SIYO MZALENDO. WAKEUP AND SNIFF THE AIR. NA USISAHAU HAO HAO WALIOKO BONGO NDIO WANAOIIBIE NCHI AU WANANCHI ANS SIO ALIYE UINGEREZA. DOH!!!!

    WEWE SHANGAA TU, KWANI MKONO MTUPU HAULAMBWI

    ReplyDelete
  16. wewe mshamba namba(1,2)mnatokea wapi namunaishi katika dunia gani hamueleweki hahahahahahahahah kaenitu naujingawenu watu wanakula marahayao kwautulivu kabisakabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...