Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akifuatilia kwa makini majadiliano ya Mkutano wa pili  uliokuwa ukijadili  uandaaji wa malengo mpya ya maendeleo endelevu ( SDGs). 
Mkutano huo ulifanyika kwa siku tatu  hapa Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa  na  ni mmoja wa milolongo ya mikutano ya majadiliano yanayolenga kuunda malengo hayo endelevu ili kuendeleza maudhui ya malengo ya Milenia ambayo mipango yake itafikia tamati Mwaka 2015. 

Tanzania ni kati ya nchi Thelathini ambazo zimechaguliwa kuongoza majadiliano hayo. Akichangia   majadiliano hayo, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na mambo mengine alisisitiza kwamba malengo mapya ya maendeleo  pamoja na kuzingatia mihimili mitatu ya ajenda za maendeleo yaani uchumi,  jamii na  mazingiria,  suala la kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini lazima liwe lengo kuu katika malengo hayo mapya.Nyuma ya Balozi, Ni Afisa Ubalozi Mwandamizi, Bw.  Modest Mero

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...