Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi. Margaret Thatcher maarufu kama "Iron Lady" amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 87.
Watoto wa marehemu Sir. Mark na Bint Carol wamethibitisha kuwa mama yao
Margaret (Baroness) Thatcher amefariki leo asubuhi na alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa "Stroke".
Marehem Margaret Thatcher alikuwa waziri mkuu wa Uingereza kuanzia 1979-1990,
katika kipindi cha utawala wake alikuwa akilumbana sana na nchi changa zinazoendelea kwa
ajili ya kuvutia maslahi ya Uingereza,kitu ambacho viongozi wa nchi nyingi za jumuiya ya madola hawakukubaliana naye.
Lakini kwa nchi yake atakumbukwa kuwa
ni kiongozi aleyesaidia sana kunyanyuka kwa uchumi wa Uingereza katika enzi za utawala wake.
Habari zaidi zitafuata baadaye
Tangulia kwa amani mama Thatcher.Poleni waingereza kwa kumpoteza mama huyu.
ReplyDeleteKipindi anatawala uingereza,kule marekani kulikuwa na Reagan,na kule Africa ya kusini kulikuwa na kaburu Botha ,watatu hawa misimamo yao kwa mtu mweusi ilikuwa haipishani walikuwa kinyume kabisa na mtu mweusi.
Jana katika mitaa ya UK walikuwa wakisheherekea kifo cha "Iron Lady"!!
ReplyDeleteRIP
ReplyDeleteHere in ma country we neither have Iron ladies nor Iron men. Most of those supposed to show the way are bagasse! or midebwedo. No rule of law.