Habari kutoka Liwale, mkoani Lindi, zinasema kwamba hali si shwari wilayani humo usiku huu kufuatia fujo kubwa zinazofanywa na wanaodaiwa kuwa wakulima wa korosho wanaodai malipo yao.
Nyumba nne inasemekana zimeshachomwa moto na ng'ombe kadhaa wamechinjwa na watu hao. Polisi wameshawasili eneo hilo na mabomu ya kutoa machozi yameanza kurindima katika harakati za kutawanya watu hao.
Habari hizo zinasema nyumba mbili za Mbunge wa Liwale na Mbili za mwenyekiti na makamu wa Umoja AMCOS zimechomwa moto, wakati ng'ombe wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya na za meneja wa Ilulu Union wamechinjwa.
Tutaendelea kwuajulisha zaidi kadri habari zitavyotufikia...
Habari hizo zinasema nyumba mbili za Mbunge wa Liwale na Mbili za mwenyekiti na makamu wa Umoja AMCOS zimechomwa moto, wakati ng'ombe wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya na za meneja wa Ilulu Union wamechinjwa.
Tutaendelea kwuajulisha zaidi kadri habari zitavyotufikia...
Nafikiri haki iangaliwe; suluhisho liwe la yeyote anayetaka kununua korosho anunue. Serikali iseme na isimamie kima cha chini cha bei ya korosho ili kulinda maslahi ya mkulima/Mtanzania.
ReplyDeleteStakabadhi ghalani ina kasoro nyingi sana na yawezekana ikpo kwa ajili ya maslahi ya watu wengine (speculation); kwa uhalisia inafanyakazi hivi: mkulima anapeleka korosho ghalani, analipwa nusu au hata chini ya nusu na hela nyingine baadae korosho zikiuzwa.
Korosho zinakusanywa na vyama vya msingi. Hivi vyama vya msingi wanapeleka hizi korosho kwa Ilulu ambao ndio wenye mamlaka ya kuuza.
Ilulu hawa wanauza kwa mnada kwa wateja ambao hawaruhusiwi kwenda kununua moja kwa moja kwa mkulima.
Miaka ya nyuma kabla ya 2011 yasemekana wateja wanaonunua kwa mnada kweli walikuwa wanashindana katika ununuzi pale mnadani. Lakini baadae yasemekana walijipanga na wakawa wamejipangia bei tayari ambayo hawaipandishi na hawaishushi.
Kidogo hapo Ilulu ambao wanakopa pesa toka NMB yawezekana wanakula hasara na hawawezi kulipa kwa wakulima.
Kama sikosei mfumo huo ndio uliokuwa unatumika kule Kilimanjaro na Arusha katika ununuzi wa kahawa; lakini ulionekana haufai na hauna maslahi kwa wakulima.
Kama nilivyoeleza hapo mwanzo; suluhisho ni kwamba wanunuzi waende moja kwa moja kwa wakulima wanunue bila kuwa na wakala hapa katikati.
Hali za wakulima kule liwale ni za kusikitisha sana; korosho zipo lakini hela hakuna na hali zao kimaisha ni mtihani. Umeme hakuna japokuwa wako kama maili 80 toka Nachingwea ambapo umeme wa gesi upo.
Kuhusu uchomaji wa nyumba na mengineyo; nafikiri ni matokeo ya haki kutotendeka kwa muda mrefu. Kwa sababu yawezekana wananchi wamepeleka malalmiko yao kwa miaka nenda rudi lakini hakuna ufumbuzi. Hapo mkulima atafanyanye?
Na huenda katika nyumba zilizochomwa yawezekana wamiliki wa hizo nyumba wanahusika moja kwa moja na mfumo mbovu wa ununuzi wa korosho na ambao ni kandamizi kwa Mtanzania; yani kama ukoloni na tena twaweza sema heri ya ukoloni.
Cha msingi ni kuwasihi Wanaliwale wasifanye vurugu; washikamane na watafute njia mbadala ya kuuza korosho zao. Yani msimu ukija watu wote wagomee kuuza korosho kwa mfumo huo uliopo. Korosho hata moja wasiuze kwa kupitia mfumo huo.
Yawezekana wakulima wanakuwa katika hali mbaya sana kiuchumi katika kipindi cha msimu wa korosho; lakini Waswahili tunamsemo wetu baada ya dhiki ni faraja.
Kila la kheri Watanzania na Muumba awajaalie viongozi wetu kutenda haki kwa wanaowaongoza bila kuwa na chembe yeyote ya upendeleo kwa yeyote yule; na Aliyetuumba atuendelezee amani nchini kwetu.
Chonde chinde viongozi na watendaji mbalimbali hapa nchini tendeni haki. Tanzania ya leo si ile ya zamani ya "yes people". Tazama ilivyowagharimu viongozi hawa wa Liwale. Wamshukuru Mungu uhai wao umenusurika. Hili liwe fundisho kwao na wengine wenye tabia kama zao.
ReplyDeleteMdau wa kwanza umefafanua vizuri sana.
ReplyDeleteKuna kila sababu kufanya mabadiliko na kuvunja udhalimu huo ktk Mfumo wa Masoko.
Lohhh, kwa mwendo huu hivi pana uwezekanao tukatoa hali bora kwa watu wa chini kama hao Wakulima wa Korosho Liwale?
Chonde-chonde Wtz na viongozi wenu "Amani Amani Amani". kwani mkipandacho ndio mkivunacho.
ReplyDelete