Barabara hii ni ya kutoka Singida kuelekea Shelui mpaka Igunga Mkoani Tabora,na hapa ni katika kijiji cha Ntondo kilichopo Mkoani Singida.Shukrani kwa wadau wote waliojaribu kujibu Chemsha Bongo hii ambayo haikuwa na Zawadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Weraaaa weraaaa..Nimepata Tabora:Sheluhi-Tinde!!!Nimepita kama mara 5 hivi naendesha gari mwenyewe.Nilikuwa nasubiri jibu

    ReplyDelete
  2. Ashsante -
    Hicho nacho kinaweza kikaboreshwa kiwe kipengele cha kawaida humu ili kuwakutanisha wadau katika kujizoeza Jiografia ya nchi yetu (hata hivyo huu ni mtazamo wangu binafsi)

    Napendekeza:
    1. siyo lazima swali lije kilasiku, inaweza ukafanya labda mara moja kwa wiki au vinginevyo;
    2. unaweza ukatengeza vipengele kadhaa kwa swali moja na kutoa alama kila kipengere mfano-Mkoa/mpaka kati ya mikoa (10%)wilaya(20%)kijiji (30%)barabara/mtaa (50%)au unaweza ukaona namna bora zaidi ya kufanya kuhusu kutoa alama kwa vipengele kama hivyo;

    Kwanini napendekeza hivyo?
    1. kama mitihani ingekuwa inatungwa kwa swali moja tu lenye alama 100% wengi tungefeli;
    2. mchanganuo wa vipengele unatoa hamasa ya mtu kujaribu, kwavile anajipa moyo ikiwa ntashindwa kipengele x chenye ala (sema 20%) huenda nkapa kinginecho na kinginecho na jumla ikawa angalau ya kuridhisha n.k.

    Namna nyingine:
    1. Unaweza ukatengeneza muundo wa maswali ya "chahua jibu lililo sahihi zaidi" nayo inaweza ikafanya kazi njema tu kwa aina hii ya mzswali;
    2. "kweli au siyo kweli" nayo inaweza kutumika japo inahitaji ubunifu wa namna yake sana kutunga maswali namna hii-hasa kwavile wadau wanaweza kufanya "guess work" ambayo mtu akipa ni ngumu kujua kama kabaatisha au Jiografia iko mahali pake (nao ni mtazamo tu)

    Hitimisho:
    - Ni kipengele kizuri, kinaweza kuboreshwa.
    - Ahsante, kwa mara nyingine.

    ReplyDelete
  3. Njiapanda kulia ni ya kuingia Iguguno

    ReplyDelete
  4. Unashuka kuingia mjini Chalinze kutokea Wami

    ReplyDelete
  5. umetoa wazo zuri mdau, naunga mkono Hoja

    ReplyDelete
  6. Hapo unaingia Wilaya ya Mwanga

    ReplyDelete
  7. Inatoka inakotoka; inakwenda inakokwenda!

    Ubishi wa nini?

    ReplyDelete
  8. hii naona kama kwetu 'mkanyageni" Tanga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...