Hapa ndipo alipopigwa risasi na kuuwawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mzee Abeid Amani Karume wakati akicheza bao na marafiki zake katika makao makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja. Matundu yanayookekana kwenye ukuta ni ya risasi zilizomiminwa na muuwaji ambaye naye aliuwawa na walinzi wa Mzee Karume, mnamo Aprili 7, 1972. Chini wanafunzi wakiiangalia sehemu hiyo ambayo haijaguswa wala kuondolewa kitu na  imewekwa uzio kuihifadhi kama kumbukumbu

Sanamu ya Mzee Abeid Amani Karume ikiwa mbele ya Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal,wakati tukifanya kumbukumbu ya Karume-Karume Day naomba wimbo wa ZANZIBAR kwenye "Ngoma azipendazo Ankal"ingawa maneno mengine kwenye wimbo huu yameshapitwa na wakati(?)

    http://www.eastafricantube.com/media/24978/Sipho_Mabuse_-_Zanzibar/

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...