Kuna vicheko vingine eh? 

Wataalamu wa mambo ya afya wanasema kucheka ni afya! sijui kama kweli au lah?
Nchini india kuna  vilabu vya kufanya mazoezi ya kucheka,pia katika  nchi nyingi kuna  wasanii wachekeshaji (Comedy)wanaofanya vituko kuwawezesha wanadamu wengine wacheke,inamaana kucheka ni tiba ya kuondoa fikira mbaya katika nafsi au? na wasanii wetu wa vichekesho nao ni madaktari.

 Lakini tunajiuliza hivi kila anaeonyesha meno anacheka au? kama kamanda Ras Makunja wetu (pichani) juzi juzi alikua studio kupika nyimbo akafumwa akicheka sana sana kiasi ya watu waliokuapo pale walikua wakijiuliza hivi kicheko cha kamanda meno nje! ni kicheko kweli au ? tukae mkao wa kula kusikia ujio wa vitu vipya kwa siku za usoni.
lakini acha tuendelee kupata raha za wikiendi at ffu camp www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kicheko hicho cha Simba S.C ni cha majuto kwa kuzidi kudidimia ktk Ligi Kuu ya Tanzania.

    Na sasa kwa kukenua huko kwa memo kwa Mnyama ni dalili ya maumivu ambapo ampigwa Bao 5-0 na Yanga S.C

    !!!

    Mpo hapo Simba?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...