BWANA HASHIM NA MAI WAIFU WAKE KURUTHUM MAYA WAMEKULA KIAPO KIPYA BAADA YA MIAKA 26 YA NDOA.HARUSI ILIFANYIKA THE HAGUE,  HOLLAND.
BWANA HARUSI BI HARUSI NA BWANA HIJA.
KURUTHUM MAYA BI HARUSI.
 MAYA WIFI YAKE NA MWANAE MAYA.
MAHARUSI NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI.
MAHARUSI NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mmependeza! Hongereni sana miaka 26 si haba katika ndoa.

    ReplyDelete
  2. Sasa hapa mbona hatuelewi ? yaani wapo katika ndoa miaka 26? harafu wamekula kiapo tena yaani wamefunga ndoa tena bomani au? ndio kusema miaka 26 ya ndoa yao ilikua mbovu mbuvu au?
    Tunaomba mkituma habari hapa katika baraza la jamii wekeni mambo wazi au hadharani

    ReplyDelete
  3. Siunajua kiswahili kina matao. Hayo ndio mambo hadharani

    ReplyDelete
  4. Annon hapo juu huelewi nini? Wamekula kiapo tena. Kiswahili kigumu?

    ReplyDelete
  5. Wewe anony 08:05
    ujamuelewa mtoa maoni namba 2,kauliza vitu vya msingi,unaposema wamekula kiapo tena ! unapotosha maana ya ndoa iliyofungwa miaka 26,kwa miaka 26 iliyopita wanandoa walikwisha kula kiapo tayari mbele ya sheikh au mfunganishaji ndoa.inapoaandikwa wamekula kiapo tena inamaana kiapo cha mwanzo kiliyumba au ?
    Lazima ujue maana ya ndoa kuwa ni mkataba wawapendanao kimaisha,sio mkataba wa kupanagisha nyumba kuwa unaweza ku renue,mkataba ukumalizika.
    hapa lazima tuelemishane kuwa ndoa zetu za kidini au za kitanzania hazitambuliki ughaibuni na inapobidi kutambulika basi lazima wanandoa wafunge tena katika ofisi za serikari,hili linaweza kuelimisha umma. kwa wengi tupo katika safari za kutafuta maisha basi lazima tuelekezani mambo yanavyokwenda huko ughaibuni.kuliko mkitumia lugha za njia ya mkato heti wamekula kiapo tena ! maana ya kiapo ni kuilishana YAMINI kwa watu ambao wasio aminiana.

    ReplyDelete
  6. Hongereni saaana!

    Kwa zama zetu hizi za Ndoa za kuhesabu siku watu wanaoana Mwezi Shaabani kabla ya Ramadhani ile inafika Mfunguo Mosi baada ya Iddi Talaka imetoka!

    Miaka 26 ya Ndoa sio mchezo hawa wamehitimu wanastahili pongezi.

    ReplyDelete
  7. Mjomba Hashim na shangazi kuruthum nawapa hongera sana. nawaombeeni kwa mungu awape mafanikio makubwa katika ndoa yenu. (John wa Dublin, Republic of Ireland)
    .

    ReplyDelete
  8. hongera sana uncle and aunt.

    ReplyDelete
  9. Ndugu zangu hongereni sana. kuishi miaka 26 sio mchezo.nawatakia maisha marefu. (john , dublin ireland).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...