Mabloga wakiwa wamembeba juu mwanalibeneke na mshambuliaji mkabaji Sufiani Mafoto baada ya kufunga penati  ya mwisho na ya ushindi  iliyowapeleka fainali za michezo hiyo iliyofana sana katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam jana.

Baada ya kufanya vyema katika TBL Media Day Sports Bonanza, Tanzania Bloggers United hivi sasa wanajipanga ili kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na NSSF Cup mwakani.

Pia wanapanga kufanya ziara kibao ndani na nje ya nchi, hasa Marekani ambako wanapanga kupambana na Yanga na Simba za DMV.  Katibu wa muda wa timu hiyo Sufiani Mafoto ametoa shukrani tele kwa kampuni ya SAPHIRE kwa kujitokeza kama wafadhili wake wa  kwanza. Amewashukuru pia waasisi wa wazo la kuwa na timu ya mabloga ambao ni wanalibeneke Francis Godwin wa Iringa na Lukaza wa UDOM ambao wanaingia kwenye vitabu vya historia ya tasnia ya blogu kama waanzilishi wa hili.
 Mshauri wa ufundi wa Tanzania Bloggers United, Ankal, akitoa maelekezo wakati wa mapumziko. Ankal alisikitika sana baada ya kiungo Maggid Mjengwa kucheza nusu ya kwanza tu na kuondoka kwenda kuendelea na kazi. Hata hivyo pengo lake lilizibwa na Mroky Mroky na Francis Dande.
 Kikosi cha Tanzania Bloggers United
 Kipa wa Tanzania Bloggers United Othman Michuzi akipongezwa kwa kazi nzuri
 Mshauri wa ufundi, Ankal, akiwa na furaha kwa matokeo mazuri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankali Michuziktk Picha ya Chini kama Mhe. Rage wa Simba S.C aliuliwa kwani ninacheza Namba ngapi hadi nijiuzulu Uonngozi Msimbazi?, Je na wewe Ankali Mwana Yanga S.C umecheza Namba ngapi kwenye Timu ya Wanalibeneke hadi uchekelee Ushindi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...