Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr Nasor Ally Hamid akisoma
hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Uzinduzi wa wiki ya Chanjo
ambapo Mkoa wa Lindi kwa Mwaka 2012 imeshika nafasi ya Kwanza
Kitaifa..Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika kata ya Mingoyo
shule ya msingi Mnazi mmoja Lindi.
Mtoto Fatma Issa akipewa chanjo na Mkuu wa Wilaya ya
Lindi katika Uzinduzi wa WIKI YA CHANJO.
Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Lindi,Dr Sonda Yusuf akitoa
taarifa ya chanjo na changamoto zake katika Maadhimisho hayo.
Mratibu wa chanjo mkoa wa Lindi Bi Zainab Mathradas
akitoa taarifa za chanjo mkoa wa Lindi huku akitoa wito kwa akina Baba
kwenda kliniki sambamba na akina mama ili wapatiwe vipimo na chanjo
mbalimbali.
Wadau wakisiliza hotuba ya uzinduzi wa wiki ya chanjo.
Na Abdulaziz video,Lindi
MAADHIMISHO ya Wiki ya Chanjo kitaifa Mkoa wa Lindi yamezinduliwa leo
huku Mkoa huo ukishika nafasi ya kwanza Kitaifa kwa kuvuka lengo la
kutoa chanjo mwaka 2012.
Maadhimisho hayo yalizindiliwa jana kitaifa mkoani Pwani na Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete yatatumika katika kuhamasisha na kuelimisha
jamii kuhusu umuhimu wa chanjo pamoja na kuwasisitiza wazazi
kuwapeleka watoto kwenye vituo vya afya ili kupata huduma ya chanjo.
Akizindua Maadhimisho hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mkuu wa
wilaya ya Lindi,Dr Nasor Ally Hamid alieleza kuwa Mpango utakaosaidia
kutokomeza magonjwa kama vile kifua kikuu, kifaduro, polio, nimonia,
pepopunda, homa ya ini na uti wa mgongo pamoja na kuzuia vifo vya
watoto.
Pamoja na kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwa kiasi kikubwacha
kuwapatia chanjo watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja kwa
zaidi ya asilimia 80 ambao wako katika hatari ya kupata maambukizi ya
magonjwa hayo Wito umetolewa Kwa Akina Mama kujitokeza kupata chanjo
hizo kufuatia kubainika kuwa watoto hawajapata chanjo na wengine
kutokamilisha chanjo hizo.
Akiongelea Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Okoa maisha, jikinge na
ulemavu Pata chanjo.’Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Dr Sonda Yusuf
Shaban alizitaka Halmashauri kuongeza ununuzi wa gesi na majokofu ili
kusaidia uzuiaji wa magonjwa kupitia chanjo mbalimbali
Sambamba na Uzinduzi huo.
Mratibu wa Chanjo Mkoa,Bi Zainab Mathradas
alitoa wito kwa akina mama kuacha kuzalia Nyumbani ikiwa pamoja na
akina baba kuhudhuria Kliniki kwa Vipimo mbalimbali ambavyo vimeanza
kutolewa sambamba na akina mama wajawazito.
Mkoa wa Lindi una jumla vituo 238 vya huduma ambapo kati ya hivyo ni
197 tu vinavyotoa huduma za chanjo kiwango cha utoaji huduma hiyo
ikiongezeka kwa asilimia 7 na kuvuka lengo la kitaifa kwa asilimia 98
badala ya 80 iliyopangwa
Lindi? haiwezekani! wa mwisho amekuwa wa kwanza? siamini!
ReplyDelete