Pamoja na kwamba katika eneo hili la msitu lililopo maeneo ya Shelui mkoani Singida,kuna vibao vinavyokumbusha ukuhimu wa kutunza misitu (kama kionekanavyo pale mbele),lakini bado watu wa maeneo hayo wanaendelea kukata miti ili kupata kuni na wengine kupata mkaa kwa ajili ya biashara au matumizi binafsi.hali hii inaonyesha dhahiri kuwa somo na utunzaji wa mazingira bado halijawaingia kisawasawa wahusika,kama Kamera ya Globu ya Jamii ilivyoweza zinasa taswirazz hizi.
Home
Unlabelled
UTUNZAJI WA MISITU BADO NI KITENDAWILI KATIKA BAADHI YA MAENEO HAPA NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
GREEN ENERGY REVOLUTION:
ReplyDelete(Mapinduzi ya Nishati ya Kijani)
Ni aibu kubwa sana na kiwango kikubwa cha uvivu wa kufikiri kushindwa kutimia VINYESI VYA NG'OMBE, MBUZI na KONDOO kuzalishia Gesi ya Kibaolojia (BIOGAS) kwa Mkoa wenye wingi wa kutosha wa mifugo kama Singida.
Hivi ktk Wilaya zetu hakuna watu kama Afisa Nishati wa Wilaya?
Pana hitajika GREEN ENERGY INITIATIVES za haraka sana Mkoani Singida ukizingayia ndio Mkoa ambao umaethirika sana na uharibifu wa mazingira huku ukiwa kiasili ni mkame zaidi nchini.
Wananchi wenye mifugo mingi watumie vinyesi vya mifugo ili kuzalisha gesi ya Kibaolojia (biogas) ili kuzalisha nishati kwa matumizi ya kupikia na kuwashia taa za majumbani na kuinusuru misitu na mazingira.
Muwasiliane na hawa hapa ili walete miradi hii:
1.TBPP-Tanzania Biogas Partnership Program.
2.SNV World-HIVOS ,Tanzania.
Acha siasa, vigogo wenyewe wa mazingira wakitoka safari hupakia magunia ya mkaa kwenye ma VX sembuse hao wanyonge. Watu wa mtwara tupeni gesi yenu tupikie kama sisi tunavyowaleteeni umeme wa kidatu muutumie.Chenu chetu, chetu chenu.
ReplyDeletewacheni kuchonga sana kumbukeni tulipotoka asilimia kubwa ya watanzania tumekuwa kwa kupata matumizi ya hizo kuni
ReplyDeletewaacheni watanzania wenye nchi ambao ni walalahoi wajisaidie kimaisha kwa njia hizo walizoachiwa na mwalimu
msifikiri kila mtanzania kapata elimu ya kumuwezesha kukaa ofisini au kugombania ubunge
kumbukeni maisha ya watanzania alisi ni magumu sana na wanapata shida sana kuweza kujiendesha kimaisha
kama mnajuwa kuongea wapiganieni hao walalahoi kwa serikali ili iweze kuwasaidia kimaisha......lakini msikae kuwalaumu pasipo na point
mdau
mahakama kuu ya dunia.
Wataalam mnatakiwa muwe karibu na wanannchi nyote mmekimbilia mjini dar es salaam,maelezo matupu bila ya vitendo hayatosaidia toa mfano hai wakujitolea kuokoa TAIFA lako,asanteni mdau bwegenaz
ReplyDeleteHivi utatunza misitu wakati una njaa??
ReplyDeleteHiyo picha ya juu hizo ni kuni tu za kawaida. Miti imekaukia porini.
ReplyDeleteWa chini sawa uharibifu, lakini wafanyeje waibe? serikali ndo haina mipango mizuri na wananchi wake. Wachache wanaweza kutumia moto wa umeme na gas je wengine wapikie nini? TAFAKARI CHUKUA HATUA
Wanaouza mbao na magogo nchi za nje na kula rushwa kwa kuwapa leseni za kukata miti na kuiuza nje ya nchi mbona hawakupigwa picha?
ReplyDeleteAcheni walala hoi nao wafaidi rasilimali ya mictu. Madini hawanufaiki nayo na misitu nayo? Mnataka wapikie nini? Mtanzania wa nanjilinji anaweza kununua gas apikie?
ReplyDeleteNYIE KWANZA MNAOZUNGUMZIA KUHUSU SUALA LA MAZINGIRA NAWAONA KAMA WANAFIKI VILE,,HAPO BONGO/TANZANIA ASILIMIA 100% WANATTUMIA MKAA,AU MKAAA AKIWA NAO MASIKINI NDIO UHARIBIFU UNAONEKANA TU,,NIAMBIE WEWE UNAYEZUNGUMZIA SUALA ZIMA LA MAZINGIRA ,SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI SI HUWA MITI INAPANDWA LKN NI NANI ANAFUATILIA.UMASIKINI WA MTANZANIA WA KAWAIDA NIMKUBWA SANA WENGINE HATA MKAA HUO HAWAUPATI UMESHAKUWA GHALI KWA SASA.HAPO WAMBIENI TANESCO WATOE UMEME WA UHAKIKA NA WA BEI NAFUU HUKU SERIKALI IKIWAWEZESHA WANA NCHI WAKE KUTUMIA UMEME HUO NA KUPATA SEHEMU YA KUPATA KAZI YA KULIPIA UMEME HUO.MPAKA MUDA HUU HUKO VIJIJINI KUNA SEHEMU NYINGINE WATAPELEKEWA UMEME NA KUTUMIA HAWATOTUMIA,KWANI WENGI HAWANA KAZI YA KUPATA HELA KILA MWEZI SHUGHULI ZAO NI KILIMO TU NA WANAPATA HELA KWA MSIMU,HIVYO HATA HUO UMEME ASILIMIA KUBWA WATAUANGALIA MASHULENI NA KWENYE MAZAHANATI TU.SERIKALI KABLA YA KUPELEKA UMEME HUKO KWANZA IANGALIE WATUMIAJI WAKE.
ReplyDeletemdau hapo juu atwambie "initial cost"(gharama za kuwekeza) ili kupata nishati itokanayo na "biogas". Nijuavyo mimi si chini ya dollar 400 kujenga mtambo mdogo wa biogas wenye uwezo wa kuhudumia kaya moja. haya sasa linganisha na kipato cha mtanzania ndipo uone ilivyo ngumu kwake kumudu gharama hizo. Tutake tusitake miti itaendelea kukatwa kwa ajili ya kuni na mkaa kama Serikali haitawekeza kikamilifu katika vyanzo vya nishati kv gas asilia, umeme wa maji, wa nuclear, makaa ya mawe, biogas, solar power na hata nishati itokanayo na upepo.
ReplyDelete