Mchungaji mtarajiwa John Shabani (kushoto) akikabidhiwa shahada yake na Askofu Kitonga (Kiongozi wa makanisa ya Redeemed duniania), baada ya kuhitimu Mafunzo katika chuo cha kimataifa cha huduma (International school of Ministry - ISOM) chenye makao makuu New York Marekani. Ilikuwa ni siku ya furaha kwa mwalimu huyo wa muziki wa injili Afrika mashariki bwana John Shabani, baada ya kuhitimu mafunzo yake hayo kwenye chuo hicho cha kimataifa. John ambaye amekuwa na ndoto za kujiendeleza sana katika elimu mbalimbali, amekuwa miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri katika chuo hicho. Mchungaji huyo mtarajiwa anategemea kujiunga na chuo kimoja huko marekani ili kuendelea zaidi na masomo yake, pia amewahasa waimbaji wenzake wa injili kuwa na mpango wa kujiendeleza ki-elimu. Mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ki-dini na serikali. Makao makuu ya chuo yaliwakilishwa na Dr. Lee kutoka Marekani.
Picha ya pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...