Na Mdau Abdulaziz Video
Abiria wanaosafiri kati ya Mtwara na Lindi kwenda Masasi na watokao Masasi Tunduru,Nachingwea,Liwale na Ruangwa mnatakiwa kuchukua tahadhali kubwa kufuatia zaidi ya Magari 50 na watu wasiopugua 300 kushindwa kupita katika kijiji cha Chipite/Mkwera kufuatia eneo hilo kujaa maji yaliyotokana na Mvua zinazoendelea,

 Eneo hilo, ambalo lilitokea mafuriko makubwa mwaka 1990/1991, limeanza kujaa maji jana, hali ambayo leo imekuwa zaidi na kusababisha msongamano.
  Taarifa zaidi tutaendelea kuwapatia kadri hali inavyoendelea huku msaada wa haraka unahitajika ili kusaidia msongamano uliopo hapo ili kuepusha maafa mbalimbali 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wengine wabishi - weka picha tafadhali

    ReplyDelete
  2. kwa kweli serikali yetu tunaomba msaada mtuangalie sisi watu wa kusini hili eneo toka mvua za elinino za mwaka 1990 mpaka leo halijategenezwa TANROAD mpo wapi na serikali za Mitaa maana wala sijui barabara ipo chini ya nani pole ndugu zangu na asante kwa taarifa kwa hiyo inabidi mtu ambaye anataka kwenda masasi kutoka lindi alipite njia ya mtwara ambayo ni mzunguko mkubwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...