Na Mdau Abdulaziz Video
Abiria wanaosafiri kati ya Mtwara na Lindi kwenda Masasi na watokao
Masasi Tunduru,Nachingwea,Liwale na Ruangwa mnatakiwa kuchukua tahadhali kubwa kufuatia zaidi ya Magari 50 na watu wasiopugua 300
kushindwa kupita katika kijiji cha Chipite/Mkwera kufuatia eneo hilo
kujaa maji yaliyotokana na Mvua zinazoendelea,
Eneo hilo, ambalo lilitokea mafuriko makubwa mwaka 1990/1991, limeanza
kujaa maji jana, hali ambayo leo imekuwa zaidi na kusababisha
msongamano.
Taarifa zaidi tutaendelea kuwapatia kadri hali inavyoendelea huku
msaada wa haraka unahitajika ili kusaidia msongamano uliopo hapo ili
kuepusha maafa mbalimbali
Wengine wabishi - weka picha tafadhali
ReplyDeletekwa kweli serikali yetu tunaomba msaada mtuangalie sisi watu wa kusini hili eneo toka mvua za elinino za mwaka 1990 mpaka leo halijategenezwa TANROAD mpo wapi na serikali za Mitaa maana wala sijui barabara ipo chini ya nani pole ndugu zangu na asante kwa taarifa kwa hiyo inabidi mtu ambaye anataka kwenda masasi kutoka lindi alipite njia ya mtwara ambayo ni mzunguko mkubwa
ReplyDelete