Nyumba hizi  ambazo tayari zote zimeshauzwa (BOFYA HAPA), ziko  eneo la Kibada. Kigamboni Housing Estate ipo Kigamboni katika eneo linalofikika kirahisi, kilomita 17 kutoka Feri. Kigamboni Housing Estate ni mradi wa nyumba 182 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo sehemu za kuchezea watoto na shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vilevile, imezingatia nafasi ya miundombinu kama vile mitaro na umeme.

Kwa mujibu wa tovuti ya shirika hilo, Nyumba hizi zenye vyumba kati ya viwili na vitatu ni mwanzo tu wa miradi mbalimbali inayoendelea nchi nzima. Uzinduzi wa Mradi huu ni chachu na dhamira ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha watanzania wanapata nyumba bora na za kisasa vile vile zikiuzwa kwa bei nafuu. Wanunuzi wa nyumba hizi wataishi kwenye maeneo kwa kuzingatia mfumo wa hati pacha (Unit titles Act 2008). Mfumo huu utawawezesha wakazi kuishi katika utaratibu wakiongozwa na sheria hiyo ambayo imeundwa kulinda maslahi ya kila mnunuzi.

Katika mradi wa Kigamboni Housing Estate, nyumba ya vyumba vitatu ina ukubwa wa 70m² huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na ukubwa wa 56m², ambapo Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwa ajili ya matumizi binafsi ya wakazi ikiwa ni pamoja na maegesho ya magari hadi matatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hongera NHC, ila sioni mantiki ya kuleta taarifa hii kwani nyumba zimeshauzwa. Kwa ushauri, endapo itatokea tena mnauza nyumba, tafadhali wekeni matangazo kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama vile radio, tv, mitandao,na hata ikibidi mabango makubwa barabarani; matangazo yenye taarifa kamili ya nyumba zitakazouzwa na bei pia. Ukitoa kasoro hii, nawapongeza tena

    ReplyDelete
  2. NHC tunaomba majibu ya madai mazito ya mdau wa kwanza hapo juu.Vinginevo na mimi nawapongeza

    David V

    ReplyDelete
  3. kuna faida gani kutangaza hii habari wakati umeshaunza je ni lini na wapi mliweka tangazo la kuunza nyumba ? na vile vile kwa naomba wakati mwingine mnapojenga nyumba na pia muuahangalia na mila na desturi ya kwetu maana nyumba ya nyumba viwili au vitatu azitoshe familia zetu na hii itafanya mtu anunua nyumba ila watu wanaoishi humo zaidi na italete maahara kwa ufupi tizma manyumba ya ubungo na ilala kwa hiii pia tujifunze..

    ReplyDelete
  4. kiukweli walishatoa matangazo ya kuanzia ujenzi wa hizi nyumba, mpaka zilivyoanza kujengwa, mpaka kufunguliwa rasmi na muheshimiwa Rais, bei n.k, na mpaka watu walikuwa wanaenda kuziona na kuchagua...yote hayo waliyaeleza at the very first stage labda kama mdau taarifa haikukufikia.

    ReplyDelete
  5. Kwanza, niungane na mchangiaji wa hapo juu, kwamba NHC walijitahidi sana kutangaza utaratibu mzima wa uuzwaji wa hizi nyumba za KIGAMBONI. Labda ni vile watanzania hatuna utaratibu wa kufuatilia habari mbalimbali. Mimi nipo nje ya nchi lakini niliweza kujua utaratibu mzima. Pia kuna clips za kipindi cha MAISHA NI NYUMBA kinachorushwa na Channel ten zinapatikana YUTUBE zimeelezea utaratibu mzima. Natumaini hii habari imewekwa hapa kuwafahamisha waliokwisha nunua juu ya hatua iliofikiwa katika mchakato wa ujenzi wa nyumba hizo.

    Pili, napenda kuipongeza NHC kwa utartibu huu mzuri ambao naona kama tutaendelea hivi basi tutegemee kufikia malengo ambayo yaliwekwa mwanzoni wakati wa kulianzisha shirika la nyumba la taifa juu ya kumpatia mtanzania wa kawaida makazi bora. Ingawa changamoto ninayoiona kwa sasa ni kwenye gharama za hizo nyumba kutokana na VAT.

    ReplyDelete
  6. Wengi wetu ni wavivu kutafuta na kufanyia kazi taarifa. Mahiri kulalamika pindi dili limeshapita. Mnaotaka nyumba mzisubiri NHC wawaletee habari. Nendeni offisini kwa mkaulize ni wapi wanajenga awamu ijayo. mnunueeee.

    ReplyDelete
  7. kusema ukweli mi niliona zile za bei kubwa tuu, za upanga, hizi za bei nafuu sikuona matangazo yake! nilisikia tuu zimekwisha!

    ReplyDelete
  8. Ni mazoea ktk Tanzania kuona kandarasi inatangazwa Gazetini huku tayari Mkandarasi akiwa ameshachguliwa zamaniii.

    Tangazo la Gazetini linatolewa ili kuondoa lawama na malalamiko ya wakata manyasi tu.

    Bongo ni kama tuijuavyo!!!

    ReplyDelete
  9. Ni kweli walitangaza lakini bei nafuu unayoizungumzia si kwa mtanzania wa kawaida . Hiyo bei nafuu iliwalenga hao hao

    ReplyDelete
  10. Wekeni pia sehemu za "parks" kwa ajili ya kupumzika na watoto kucheza pamoja!

    ReplyDelete
  11. MTEJA NHC BOKOApril 22, 2013

    NYUMBA HIZI ZILITANGAZWA SANA KWENYE TV,RADIO NA MAGAZETI NADHANI HII TABIA YETU YA KUJIKITA KWENYE TAMTHILIA NA BONGO FLAVA MENGINE YANATUPITA, HONGERENI SANA NHC, ILA NI MATUMAINI YANGU KUWA NI KWELI MUMEJENGA NYUMBA BORA NA IMARA KWANI BOKO NDUGU ZETU MUMETUCHAKACHUA KWA HERUFI KUBWA. ENDELEENI NA BORESHENI.

    ReplyDelete
  12. NHC HONGERENI, HIVI NDGU ZANGU WA BONGO MNATAKA RAHISI YA NAMNA GANI, MSINIELEWE VIBAYA MIMI NIANDIKAE UJUMBE HUU SINA HATA BANDA LA KUKU, JAMANI ANGALIENI VIFAA VYA UJENZI VILIVYO GHALI, BADO FUNDI, KUHANGAIKA NA USAFIRI NA MENGINEYO HIVI INAWEZEKANA KUPATA NYUMBA YA UHAKIKA JAPO YA VYUMBA VIWILI JIKO BAFU SEBULE N.K KWA CHINI YA MILLION 30? JAMANI NIFAHAMISHENI NIJITAHIDI LABDA NITAWEZA.

    ReplyDelete
  13. WATANZANIA MNAMAJUNGU SANA MTU HATA AJITAHIDI VIPI KUTENDA KAZI LAZIMA MUONE HAMJATENDEWA HAKI. SIO WA MIKOANI TULISIKIA NI KWAMBA TU HATUKUJIPANGA LEO WEWE MDAU WA KWANZA NA PILI MNALALAMA LO

    ReplyDelete
  14. Be I ya chini ni shilling ngap? Na naitaji maelekezo zaidi maana naitaji kununua moja ya nyumba hzo
    hongeren kwa kuleta mradi huo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...