Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi  (pichani) hatuwezi kulikwepa. Yeye  ni Mtanzania mwenye makazi yake huko Texas, nchini Marekani. 
Kabla ya kujikita huko Romi  alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale Zanaki jijini Dar es salaam chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), akiwa mmoja wa vijana wadogo wateule wa mwalimu huyo aliyebuni kundi maalumu la vijana hodari wa mchezo huo, kwa jina Bomani Brigade.

Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi huko Okinawa nchini Japan, Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga.

Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji, akiwa  ni mwalimu wa karate na yoga mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana na mwenye nidhamu.

Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni. Ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo na kadhalika  wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.
Sensei Rumadha Fundi 'Romi' (3rd Dan black belt),  akiwajibika katika semina ya karate katika Dojo ya Sugarland, Texas, nchini Marekani katika semina ya walimu wa karate (ma-sensei)  chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sensei Rumadha ni mtaalam aliyebobea kwani alianza mazoezi akiwa kijana mdogo na tangu wakati huo hajasimama amekuwa akiendelea kujiboresha kwa kufanya mazoezi ya karate kwa miaka mingi kwa hiyo ana uzoefu, ushupavu na ujasiri ulioupata kwa mazoezi ya dhati, pia ni mwalimu mpole mwenye moyo wa kujitolea pamoja na kusaidia watu wengine..... watanzania tutanufaika sana na wataalamu kama Sensei Rumadha fundi!

    ReplyDelete
  2. Sensei Rumadha anakubalika kimataifa,
    Karate na Yoga ni mtaalamu anayeweza kuelemisha umma

    ReplyDelete
  3. Ankal,haya ndio mambo,kumbe yule freddy macha sio mwalimu wa Yoga au karate? bali alidandia tu !kumbe watalaamu wenyewe waliobobea katika Yoga na Karate na kutambuiwa kimataifa wapo? Big Up Sensei Rumadha Fundi

    ReplyDelete
  4. nimekumbuka enzi za gojirawa okinuu enzi zetu palea zanaki sec school michuzi Bernad King dom yuko wapi?

    ReplyDelete
  5. Sensei Rumadha kifaa cha kazi tena ni fahari ya watanzania kujivunia

    ReplyDelete
  6. Shemeji yangu huyo, Mnyamwezi kiukweliukweli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...